Ads (728x90)



 
Shilingi  milioni 250 zilizopaswa kutumika kwa ajili ya chakula kati ya Rais Dkt.Magufuli na wabunge zimeelezwa kutumika kwa ajili ya kununulia vitanda 500 vya Hospitali ya TAIFA Muhimbili.
Kwa nia njema kabisa rais ameamua kufanya maamuzi hayo akiamini kuwa anachokifanya kitaisaidia jamii ya wengi wanaotaabika hospitalini kwa kulala chini na baadhi yao kukosa dawa, Big Up Mr President!!!!.
Rais Magufuli alihutubia bunge siku ya Ijumaa Novemba 20 ambapo baada ya kumalizika kwa hotuba ya Spika wa Bunge Job Ndugai alisikika akiwatangazia wabunge kuhudhuria chakula pamoja na rais hiyo ni baada ya kupata picha ya pamoja.
Imeelezwa kuwa rais aliamua gharama za chakula hicho zilizofikia shilingi milioni 250 zielekezwe kwenye huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya dawa na vitanda, Shout Up Mr President kwa huruma zako kwa watanzania wenye matatizo.
Siku ya pili baada ya kutolewa taarifa hiyo wagonjwa katika hospitali ya muhimbili walishuhudia vitanda 500 vikiletwa hospitalini hapo.
Swali linakuja ,Jee!!  ni utaratibu upi umetumika kwa ajili ya kupatikana kwa vitanda hivyo?sheria za manunuzi kwa ajili ya mali za serikali zimefuatwa?
Vitanda hivyo vimetolewa wapi kwa haraka namna hiyo na wazabuni wangapi walishindanishwa  kwa ajili ya kazi hiyo ya usambazaji wa vitanda hospitalini hapo na hatimaye mmoja akapatikana  kama ambavyo taratibu za zabuni za serikali zinavyotakiwa?


Post a Comment