Ads (728x90)


Baadhi ya abiria wa Basi la Newforce walioibua tafrani kwenye Kituo cha Mzani Uyole jana asubuhi

Add caption

Basi la Newforce likiwa katika kituo cha mizani Uyole jana



Kituo cha Mizani Uyole jijini Mbeya

Moja ya gari likishindwa kupita kwenye mizani ya Uyole baada ya kuwekewa mawe na abiria wa Basi la New Force

Kipimo cha Mzani wa Uyole kikisomeka 3500 baada ya shinikizo la kurudia kupima mara ya pili ambapo awali ilisomeka 7750

Msimamizi wa kituo cha Mizani Uyole ambaye aligoma kuwaonesha kipimo wafanyakazi wa Basi la New Force ambao walidai kipimo kilichoelezwa na msimamizi huyo hakisemi ukweli
 
ABIRIA waliokuwa wakisafiri na Basi la Newforce lenye namba za usajili T 520 CXE linalofanya safari kati ya Kyela na Dar es salaam walilazimika kuweka mawe kwenye kituo cha mizani Uyole wakipinga kitendo cha wafanyakazi wa kituo hicho kulitoza faini basi hilo kwa madai ya kuzidi uzito
Waliibua tafrani wakionekana wakiwa na hasira  wakibeba mawe na kuyaweka kwenye njia ya kupita kwenye mizani ili kuzuia magari mengine yasipime kwa kile walichodai hadi hapo watakapooneshwa uzito unaodaiwa kuzidi wa Basi hilo.
‘’Tunataka watuoneshe uzito wa hii gari wanadai limezidi uzito wakati ndani ya Basi tupo abiria 41 na hili basi linabeba abiria 57,’’alisema mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la Angelina Basiku anayesafiri kuelekea jijini Dar es salaam.
Naye abiria aliyejitambulisha kwa jina la Ephraim Mwankenja alisema kuwa kitendo hicho ni wizi wa wazi wa baadhi ya watumishi wa mizani katika maeneo mengi ambao hutoza faini kinyume cha taratibu.
Mwankenja alisema iwapo Basi linakuwa limezidisha abiria au mizigo uzito wake unaonekana na kuwa kitendo cha  kusema Basi hilo limezidi uzito wakati lina abiria wachache na halina mizigo ni kitendo kinachotia mashaka utendaji wa wafanyakazi hao.
Hata hivyo alisema kuwa kitendo hicho mbali ya kuwa na dalili ya wizi wa wazi pia kinaleta kero na usumbufu kwa abiria wanaohitaji kusafiri kwa usalama.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mwalukuta alisema kuwa yeye amekuwa anasafiri mara nyingi na magari kuelekea Dar es salaam na kuwa iwapo Basi limebeba mizigo mingi au kuzidisha abiria uzito huongezeka kwenye mizani na kwamba ndani ya basi hilo siti nyingi ziko wazi.
Mkazi wa Uyole aliyejitambulisha kwa jina la Michael Somo alidai kuwa kituo hicho cha Mizani kimekuwa kikilalamikiwa na madereva wengi ambapo limekuwa ni tatizo sugu kutokana na tabia ya kuongeza vipimo vya mizani kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
‘’Inawezekana huu ndio utaratibu wanaoutumia hawa wafanyakazi kujipatia fedha kwa njia isiyo halali, gari likizidi uzito linatakiwa kulipa fidia, gari letu ni tupu halina abiria huo uzito umetoka wapi,’’alihoji kondakta wa Basi hilo aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Paresh.
Paresh alisema kawaida uzito wa basi hilo unatakiwa usizidi GVM 23,000  na kuwa wafanyakazi wa mizani walipima uzito ambao ulikuwa mbele ni GVM 8,550 na nyuma GVM 11,100 na hivyo kutakiwa kulipa faini sh. 36,000 na kwamba hata hivyo walipofika kituo cha Makambako wamepima tena uzito ambao umesomeka mbele GVM 7,400 na nyuma GVM 11,100.
Kwa upande wake Yuhai Chen ambaye ni msimamizi wa mabasi ya New Force Nyanda za Juu kusini alisema kuwa Basi hilo hata kama lingekuwa na abiria 61 bado uzito usingeweza kuongezeka na kuwa kilichofanyika ni ujanja wa wafanyakazi hao kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
Chen aliomba ipimwe tena wafanyakazi wakakataa na kudai kuwa kompyuta yao ilikuwa mbovu na kuhoji kuwa iwapo kompyuta yao ni mbovu inakuwaje wanatoa huduma.
‘’Huu ni ubabaishaji wametupimia wanakataa kurudia kutupimia wakidai kuwa kompyuta ni mbovu, inawezekana wanaibia watu kwa kutoa huduma kwa kompyuta mbovu’’alisema Chen.
Msimamizi wa kituo cha Uyole alipoulizwa tatizo hilo alisema kuwa yeye hana mamlaka ya kutoa maelezo juu ya suala hilo kwa kuwa si msemaji wa TANROAD ambapo Mkuu wa wahandisi wa TANROAD ambaye jina lake limesomeka kupitia namba yake ya simu ya mkononi jina la Boniface Mkumbo alidai kuwa yupo njiani kufika eneo la kituo.
Basi hilo liliondoka majira ya saa 5:00 katika kituo hicho cha Mizani Uyole bila masharti  ambapo pia Mkuu wa wahandisi wa TANROAD Mkumbo alikuwa bado kufika eneo hilo kutolea ufafanuzi tatizo la wafanyakazi wa kituo hicho kudaiwa kuzidisha vipimo vya uzito wa magari eneo hilo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Kondakta aliyesafiri na Basi hilo kuelekea jijini Dar es salaam Abul Paresh alisema kuwa waliruhusiwa kuondoka hapo baada ya shinikizo la abiria kutaka kurudia kupima Basi hilo ambalo katika kipimo cha kwanza lililonekana limezidi  8,550 na nyuma 11,000.
Alisema uzito huo haukuwiana na mzigo wa Basi hilo na kuwa baada ya kuondoka walipima tena katika mzani wa Makambako ambapo wamepata uzito wa 7,400 mbele na nyuma 11,100.

Awali walipotakiwa kupima tena walikataa na kuwa wamekwisha pima inatakiwa kulipa faini hadi pale alipofika askari na mwandishi wa habari hizi ndipo walipopima na kukuta uzito wa GVM 7,750 na nyuma GVM 11,000.

Post a Comment