Ads (728x90)

KAZIMOTO KUPANDISHWA KIZIMBANI


KIUNGO wa Simba Mwinyi Kazimoto anasubiri kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia na kumpiga mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahiba Richard.

Kazimoto alifikishwa polisi jana ana kutakiwa kuripoti leo mchana ambapo alichukuliwa maelezo yake, upepelezi umeanza kwa ajili ya kupandishwa kizimbani.

Shirikisho la soka nchini TFF linasubiriwa kutoa tamko juu ya sakata hilo na kwamba iwapo Kazimoto atapatikana na hatia adhabu ya juu ni kufungiwa kucheza soka kwa muda wa mwaka mmoja.


Mwanahiba alipatiwa matibabu hospitali ya Mkoa Shinyanga na sasa anaendelea vizuri ambapo kampuni ya Mwananchi imetoa tamko la kulaani kitendo hicho.

Post a Comment