Haao, wameshindwa, watembeza mabakuli, kujikwamua na hili,
Haao,nini kisa cha kushindwa ilhali tuna mali na rasilimali,
Haao, waongoza kwa kubeza waongozwao ni sisi wenye duni hali,
Haao, watambuliwa kama mafisadi, wakimbiza kilicho chetu.
Haao, wako wapi waloshindwa, nchi kuiendesha, na kuishia magereza,
Haao, wangalimo katika uongozi,watumia majukwaa kuzungumza kingereza,
Haao, punde wataja kwenu, kuwaomba kura zenu wakatalieni na kuwabeza,
Haao si wema kwenu, ni mafisadi wa mali zenu hawana maana kwenu.
Haao twawataka wawajibishwe, kwa wananchi wajieleze,
Haao kwa pilato wafikishwe,ukweli waueleze,
Haao ni mafisadi dhahiri, hawapaswi kubembelezwa.
Haao wazomewe hawana maana kwetu na hata kwao wenyewe.
Wakatabahu
Malenga,
ReplyDeleteZa siku? Nimepita kukusalimia. Kusalimiana kunajenga umoja.
Kazi njema sana kaka.
Shukrani kwa kunitembelea nashkuru sana ndugu yangu kazi njema nawengoja nipite kijijini kwako maana ni muda mrefu
ReplyDeleteShukrani kwa kunitembelea nashkuru sana ndugu yangu kazi njema nawengoja nipite kijijini kwako maana ni muda mrefu
ReplyDelete