Nikifa msinililie sana,bali mtafakari mema yangu na kuyafanyia kazi na kujifunza kwa maovu yangu ili mpate kujifunza kwayo.
Nikifa jifunzeni kwa mapungufu yangu ili iwe ni mazingatio kwa kutoyarejea niliyoyafanya na iwe ni Ibra mazingatio kwa vizazi vijavyo.Nikifa msitafute kurithi mali zangu bali mwatakiwa kurithi busara na hekima zangu ingawa kila binadamu hakosi mapungufu ambayo anastahili kusamehewa kwayo.
Nikifa mnizike haraka ili nisioze nikawatia kero na kunitema mate, hakuna awezaye kunirejesha hata mkilia sana amali zangu nilizozitanguliza akhera ndiyo kinga yangu mujarabu inayoweza kuniokoa na adhabu ya kaburi.
Nikifa nifanyieni mema kwa kuitunza familia yangu,ifarijike wajione kama wako na baba yao.Walionikebehi hawatoniona tena na hata wakinisema siwezi kuwasikia na wala haitowasaidia kitu kwani kila mmoja yu njiani kuelekea nielekeako mimi.
Nikifa mnizike kuelekea kibla wala msichague ni wapi pafaa kunizika kwani makadirio ya maisha yangu ni pale nifiapo na ndipo ninapostahili kuzikwa, msikose kunifanyia mambo muhimu kwa mila na desturi za dini yangu.
Nikifa wala msihangaike kutafuta sababu za kifo changu mkakamata wachawi na vinginevyo, bali mnapaswa kujua kuwa kila kiumbe lazima kitauonja umauti, na kila mja amekadiriwa riziki yake itapatikana na mwisho wake na hata mahala pa kufia amepangiwa na aina ya kifo .
Wakatabahu
Muhimu tuhuzunike, la sivyo usitutoke,
ReplyDeleteIli chozi situtoke, labda usiondoke,
Ili tusihuzunike.
Ikibidi ututoke, muhimu tuhuzunike,
Kote tukakusanyike, kidini tukakuzike,
Machozi yatudondoke.
Kulia ni lazima kwani si mtu kama watu wote
ReplyDelete