Ads (728x90)

Jiji hili zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotoka kwenye Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).
Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia kwenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.(chanzo) www.wikipedia.org

Post a Comment

Post a Comment