Watoto Halisi wa KItanzania
Hawa ni watoto, wako kila mahali katika nchi yetu, wanahitaji matunzo wanahitaji maisha bora kama wale ambaio husoma nje ya nchi, wanahitaji matibabu na kila aina ya huduma za kijamii ikiwemo mavazi na chakula, huyu hapa ni mtoto ambaye hata hajafikiria kupelekwa shule amembeba mtoto mwenzie, mama yake na baba yake wameenda kufanya vibarua katika mashamba ya wale wenye uwezo wa kumiliki hekari nyingi, hapa ni katika kijiji kimoja katika wilaya ya Mbeya, wazazi wa watoto hawa ni wapiga kura wa mwaka 2010,Mheshimiwa Mbunge umewaona wapiga kura wako, mfuko wa jimbo kwa wabunge utawafikia watu wa aina hii, yetu macho na masikio, tutaona maana waling'ang'ania kweli kupitishwa kwa mfuko huo wa jimbo pamoja na wanaharakati kuupinga hadi machozi na udenda kuwatoka.
Post a Comment
Post a Comment