-NI KWA KUMVUA HIJAB DC
-WATAKA WAWAOMBE RADHI WAISLAMU
-KUANDAMANA NCHI NZIMA
KATIBU MKUU WA SHURA YA MAIMAMU SHEKHE PONDA ISSA PONDA
WANAZUONI wa dini ya Kiislamu wamekuja juu wakikitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuomba radhi juu ya kitendo chao cha kumvua Hijabu Mkuu wa wilaya ya Igunga Bi.Fatma Kimario kwa madai kuwa kitendo hicho mbali na kumdhalilisha Mkuu huyo ni kuudhalilisha Uislamu.Wakizungumza jana katika kipindi maalumu kilichokuwa kikirushwa na Redio ya kiislamu Redio Imaan FM inayotangaza kutoka mjini Morogoro walisema kuwa kitendo cha WanaCHADEMA kumvua hijabu Bi.Kimario ni sawa na kumvua Askofu kofia ama kumvua Sister kilemba chake ama rozali.
Akizungumza kwa njia ya simu wakati akitoa ufafanuzi juu ya sakata hilo, Katibu mkuu wa Shura ya Maimamu Shekhe Ponda Issa Ponda alisema kuwa kitendo hicho hakitaweza kuvumilia na kwamba wanapanga kufanya maandamano nchi nzima iwapo chama hicho hakitaomba radhi juu ya vitendo hivyo.Baadhi ya waumini wengine wa dini ya Kiislamu waliopiga simu walikishutumu CHADEMA wakidai kuwa kimekithiri kwa vitendo vya Vurugu na kuwa hakifai kupewa mamlaka ya kuongoza wananchi.
Post a Comment
Post a Comment