Ads (728x90)

 Tumepata Uhuru Disemba 9 mwaka 1961 zipo nchi kama yetu ambazo nazo zimepata Uhuru kwa tarehe zinazolingana na nchi yetu na hata baadhi ya nchi ambazo nchi yetu imesadia kupatikana kwa Uhuru wake ambazo leo hii wananchi wake wanaishi maisha Bora yenye matumaini.
Wakazi wa nchi yetu wengi wao ni wale wenye kipato duni ambao mbali na kuishi katika nchi yenye rasilimali lukuki na ardhi yenye rutuba na madini aina mbalimbali bado wananchi wanaishi katika nyumba za mbavu za mbwa wakikosa mahitaji na huduma muhimu za kila siku kama vile maji safi na salama na hata yanapopatikana wananchi husafiri kwa umbali mrefu kuyafuata na kushinda kufanya shugfhuli zingine za kimaendeleo.

Post a Comment

Post a Comment