Ads (728x90)

 Kwa taarifa yako haya ndiyo maisha ambayo kwa miaka mingi Walibya walitamani kuyafikia, ni punde sasa 
 Maisha haya watayafikia wataishi katika nyumba aina hiii kama waishivyo Watanzania walio wengi ambao muda si mrefu wanatarajia kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru,watadiriki kulala katika nyumba za mbavu ya mbwa na kuhaha kutafuta maji ya kisimani, kwa kuwa miundo mbinu yote imeharibiwa na majeshi ya NATO.

Akina mama wa vijijini watahaha huku na kule kutafuta riziki kwa kuwa waume zao waliuawa katika vita na nchi za Umoja wa Kimataifa NATO.Hata usafiri utakuwa ni shida watadandia magari ilhali hapo awali kila mmoja alikuwa na uwezo wa kumiliki chombo cha usafiri, pia watalima kwa mikono na kusoma kwa shida.

Post a Comment

Post a Comment