Ads (728x90)

 Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Mbeya wameibuka na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro kumwajibisha Meya wa Jiji la Mbeya Bw. Athanas Kapunga (PICHANI JUU) kutokana na kuhusika na uchochezi wa vurugu zilizosababisha mauaji Jijini Mbeya.
 Viongozi hao wa dini walimtaja waziwazi Bw. Kapunga wakidai kuwa amekuwa akiliendesha Jiji la Mbeya kisiasa kutokana na maslahi yake binafsi hivyo njia bora ya kulisafisha jiji ni kuondolewa kwa Meya huyo.Walisema kuwa Bw.Kandoro amebeba lawama zisizomhusu juu ya vurugu hizo na kwamba wao kama viongozi wa dini wana imani kubwa na uongozi na utendaji wake kutokana na historia yake katika mikoa aliyopitia.

Post a Comment

Post a Comment