(IGP SAID MWEMA)
ASKARI polisi wanne wa wilayani Mbozi mkoani Mbeya ambao majina na namba zao tunazihifadhi wanadaiwa kushiriki katika kula njama ya kutorosha gari la wizi kwa kuhongwa fedha zaidi ya shilingi milioni 2. Gari hilo ambalo awali lilikuwa na namba za IT likiwa linasafirishwa kwenda nje ya nchi lilitua mikononi mwa askari hao ambao ni askari wa usalama barabarani askari wawili wa kike (namba na majina yao zinahifadhiwa)ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama ya kutorosha gari hilo.Inadaiwa kuwa gari hilo liliibiwa katika bandari ya Dar es salaam Novemba mwaka huu na kusafirishwa hadi Tunduma ambapo baadaye likiwa na namba za bandia lilianza safari ya kurejeshwa jijini Dar es salaam kupitia jijini Mbeya kwa njia za panya huku likiwa na watu wawili mmoja wao akiwa dereva. Gari hilo lilifika katika mji mdogo wa Mlowo na kutiliwa mashaka na askari usalama barabarani wa kike (namba na majina yao yanahifadhiwa) waliwashirikisha (askari majina yao yanahifadhiwa). Imedaiwa kuwa mara baada ya mahojiano watu hao walikiri kuwa gari hilo ni la wizi na kuwaomba askari hao wachukue sh.500,000/- ili wawaachie lakini askari hao inadaiwa waliomba wapewe kiasi cha milioni 2 ambazo hata hivyo hawakuwa nazo na kuwaomba askari hao walete siku inayofuata huku gari likiwa mikononi mwa mmoja wa askari hao.Imedaiwa kuwa gari hilo lilichukuliwa na kwenda kufichwa askari mmoja wa kike eneo la Mlowo hadi siku waliyoahidiana. Imeelezwa kuwa siku ya ahadi jamaa hao walipeleka kiasi hicho cha fedha kwa askari hao na kuwaomba askari hao wawasaidie kuwasindikiza hadi nje ya mkoa ili wasisumbuliwe na askari wengine barabarani. Inadaiwa kuwa askari wawili walibaki Mlowo na askari wa kike wawili walilisindikiza gari huku mmoja wao akiliendesha na wenyewe wakiwa wamekaa nyuma ya gari.Taarifa zaidi zinadai kuwa wakiwa safarini kuli ‘save’ gari hilo walikutana na vigingi katika kijiji cha Ruanda ambapo askari wa eneo hilo walipewa 'tip' kuwa gari hilo ni dili hivyo lazima upite mgawo. Hata hivyo askari hao waliposimamisha gari hilo hawakuweza kusimama ndipo wakaanza kufukuzana askari kwa askari hadi eneo la Senjele katika daraja la treni na kuanza kuzozana wakitaka wakitaka upite mgawo wa mshiko huo. |
Post a Comment
Post a Comment