Baadhi ya wananchi wa Somalia wakiwa na msimulizi wa kisa hiki Shekhe Dormohamed Issa (Mwenye kilemba chekundu)katika ibada ya sherehe ya Idd ambayo iliwakuta nchini Somalia |
Akina mama wa Kisomali wakisubiri msaada kwa wasamaria wema wa nchini Tanzania waliotembelea Somalia. |
Wanyama na ndege wameshindwa kuhimili ukame na hivyo kupoteza maisha kwa njaa na kiu. |
Ardhi ya Somali iko katika hali hii ambapo kutokana na hali ya jangwa imepasuka na hii ni kuonesha kuwa eneo hili haliwezi kuotesha mazao ya aina yoyote. |
(Akina mama wakisubiri msaada) |
Mmoja wa wanaharakati waliokuwemo katika safari hiyo Shekhe DorMohamed Issa ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhiynurayn Kanda ya Nyanda za Juu alisema kuwa safari yao ilikumbwa na vikwazo kadhaa lakini hatimaye walifanikiwa kuingia nchini Somalia na kuwakuta Wasomali wengi wakiwa katika dhiki na mashaka. |
Shekhe Mohamed anasema kuwa maisha ya watoto na akina mama yako katika mashaka amakubwa nchini Somali kutokana na athari ya Vita hususani kundi la El Shababy ambalo limekuwa likivamia maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii na kufanya uharibifu. |
Anasema kuwa maisha ya wasomali ni duni kiasi cha kumfanya kila mtu mwenye imani ya kweli kujikuta akibubujikwa na machozi. |
Anafafanua kuwa ingawa walipata vikwazo kadhaa kuwafikia Wasomali walifanikiwa kukutana nao na kusimulia kuwa safari yao ilianzia Dar es salaam, Arusha, Namanga kisha wakafika Liboi mpakani mwa Tanzania na Kenya. |
Shekhe Mohamed anasema kuwa safari yao iliendelea hadi Nairobi na kisha Garisa Njiapanda ya Ethiopia na Kenya kisha wakafika Kaskazini ya Kenya maeneo ya Daadab. |
Anasema walisafiri huku wakiwa na tahadhari chini ya ulinzi wa askari wa Kenya ambapo huko kote walikuwa wakikwepana na makundi ya Elshababy ambao wamedhamiria kuvuruga amani na utulivu wa nchi ya Somalia na kwamba kundi hilo lilikuwa km 30 kutoka eneo ambalo walifikia. Anabainisha kuwa akina mama wa Kisomali wanaishi kwa shida huku wakitafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku na hata yanapopatikana maji huwa ni yale ambayo ni hatari kwa afya zao. |
Ndege na wanyama hujifia ovyo misituni kwa kukosa chakula kutokana na hali ya ukame iliyoikumba nchi hiyo ambayo kwa takribani miaka 20 iko vitani |
Ukame ulioikumba nchi hiyo kutokana na vita vya muda mrefu vimewafanya wanyama kufa kwa njaa kutokana na kukosa malisho. |
Maisha ya Wasomali wengi yapo maporini ambako hujisitiri katika vibanda vidogo vya miti na majani. |
Maisha ya watoto ni ya dhiki wakikosa lishe na huduma bora za afya. |
Msafarawa Watanzania waliokwenda kuwasaidia wananchi wa Somalia ambao wanateseka kwa njaa na vita. |
Msafara wa Watanzania waliokwenda nchini Somalia kutoa msaada. |
Post a Comment
Post a Comment