Na, Mwanafasihi Wetu,Brantyre-Malawi
LIPO jambo ambalo limegubika utata nchini Malawi juu ya Dkt. Hasting Kamuzu Banda halisi anayedaiwa kupotelea nchi za Ughaibuni na baadaye kupachikwa Dkt. Kamuzu Banda wa bandia ili kuficha jambo ambalo hadi sasa Wamalawi wenyewe wanatafakari juu ya utata huo.
Taarifa za
uchokonozi kutoka nchini humo zinadai kuwa utata huo uliibuka mara baada ya
wananchi wazalenda wa Malawi kuhitaji kuwaondoa watu weupe kwa kile
kilichoonekana kuwepo na unyanyasaji dhidi yao ambapo aliibuka mwanaharakati
John Chilembwe aliyejitoa mhanga kuwakomboa Wamalawi.
Chilembwe
ambaye hadi sasa anaenziwa kwa picha yake kukaa katika noti za nchi hiyo
anadaiwa kluanzisha harakati za ukombozi ambazo hatimaye zilisababisha kuteswa,
kufungwa na kuuawa kikatili na serikali ya kikoloni.
Kifo cha
Chilembwe ndicho kilichoibua hoja ya kuwepo mabadiliko na kuhitaji kuwaondoa
walowezi weusi waliojikita nchini Malawi ambayo awali ilikuwa ikiitwa Southern
Rhodesia ambapo katika harakati hizo waliibuka Madaktari wawili ambaoi ni Dkt.
Hasting Kamuzu Banda(Mwafrika) na Dkt. Richard John Amstro (mzungu)ambao
walikuwa nje ya nchi ya Malawi miaka ya thelathini wakifanya kazi ya Udaktari.
Imedaiwa
kuwa madaktari hawa wawili waliishi na kufanya kazi pamoja huku Dkt.Amstro
akiwa amepangwa na wazungu kurithi nafasi ya kuongoza Malawi mara baada ya kutimuliwa
kwa wazungu akiuvaa U-Kamuzu Banda badala ya Dkt. Kamuzu Banda halisi.
Kwa mujibu
wa uchokonozi kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya Malawi zinadai
kuwa kilichofanyika ni kumpika Dkt. Amstro kwa kukariri tabia na mila za
Wamalawi akitumia fursa ya ukaribu wake na Dkt. Kamuzu Banda halisi ambapo pia
inadaiwa alijaribu hata kuijua familia ya Kamuzu iliyopo katika kijiji cha
Kasungu nchini Malawi.
Inaelezwa
kuwa wakiwa huko ughaibuni ndugu wa familia ya Dkt. Kamuzu halisi hawakujua
kinachoendelea bali kutokana na maslahi ya nchi za Magharibi ambazo kwa wakati
huo hazikuhitajika kuishi nchini Malawi ilitumika mbinu ya kumpoteza Kamuzu
Banda halisi na badala yake kupandikizwa Kamuzu Banda feki(Dkt. Amstro)
aliyerejea nchini Malawi na kujiita Dkt. Hasting Kamuzu Banda.
Hadi sasa
hakuna anayejua alipo Kamuzu Banda halisi huku kukiwa na madai ya kuuawa na
kupotezwa kaburi lake ambapo kwa mujibu wa watoa taarifa ni kwamba tarehe
halisi ya kuzaliwa Banda(halisi) ilikuwa ni mwaka 1889 na Kamuzu Banda feki
Dkt. (Amstro) alizaliwa 1901.
Inaelezwa
kuwa Dkt. Banda halisi alienda kusomea Udaktari nchini Uingereza mwaka 1934 na
baadaye alikwenda nchini USA ambako alipata PHD na ndiko huko alikokutana na
Dkt. Kamuzu Banda feki Dkt. (Amstro).
Dkt. Amstro
alirejea Malawi akiwa kama Dkt. Hasting Kamuzu Banda na kwenda moja kwa moja
kijijini alikozaliwa Dkt. Banda halisi ambap[o hata hivyo wanafamilia wa Dkt.
Banda hawakuridhika na nasabu yake kutokana na maumbile yao kwa kuwa Dkt. Banda
halisi alielezwa kuwa alikuwa na vidole vine katika mguu wake wa kushoto huku
Dkt. Amstro akiwa na kilema hali ambayo ilikuwa ni tofauti baina ya watui
wawili hao.
Noto za Malawi zenye picha ya John Chilembwe |
Dkt. Hasting Kamuzu Banda anayedaiwa kuwa ni Mzungu |
Hata hivyo
jitihada za kidiplomasia zilifanyika hadi wanafamilia hao wakakubali kuwa ni
ndugu yao ingawa hawakuridhika ambapo alijitahidi kupeleka huduma nyingi za
kijamii katika mji huo wa Kasungu na kufanya wakazi wa eneo hilo wasahau kuhoji
nasabu ya Dkt. Amstro na hivyo kulazimika kumkubali kuwa ndiye Dkt. Kamuzu
Banda.
Katika
uongozi wake Dkt. Banda aliwaweka karibu watu kama akina John Tembo ambapo
baadaye lilizuka kundi la watu waliohoji uhalisi wa Dkt.Hasting Kamuzu Banda
kama vile Mwandishi wa vitabu Kanyama Chiume, Dunduzu Chisisa, Gwebe,Chiwanga,
Olton Chirwa, Mtangazaji Denis Liwewe, Kamungu, Aron Gadama, Chiwanga na
wengine wengi waslioamua kuikimbia nchi hiyo.
Inaelezwa
kuwa baadhi ya watu waliokuwa wakifuatilia sakata hilo kama vile Gadama na
Chiwanga walitengenezewa ajali katika barabara ya Tsisangani ambako walipoteza
maisha, na kuwa mpango huo ulikuwa chini ya kikundi maalumu cha Kimafia
kinachofahamika kama Malawi Young Pioneer ambacho kinadaiwa kuwa ni hatari
kuliko hata jeshi la Malawi.
Hata hivyo
katika utawala wa Dkt. Kamuzu Banda aliyeingia kwa ajili ya kulinda maslahi ya
Wazungu akijifanya ni Mmalawi na President wa Muyaya aliweza kuboresha hali ya
wakulima wa nchi hiyo kiasi cha kuwasahaulisha machungu waliyokuwa nayo
Wamalawi juu ya historia ya kuingia kwake madarakani.
Dkt. Banda
aliishi na kupewa mke ambaye inaelezwa hakubahatika kuzaa naye na aliyekuwa
Katibu Muhtasi wake aliyefahamika kwa jina la Cesilia Kazamila.
Dkt. Banda
alifia nchini Afrika Kusini alikoenda kwa ajili ya matibabu mwaka 1997 wakati
nchi yake ikiwa ndani ya mageuzi chini ya utawala wa chama kingine cha UDF
kilichoongozwa na mwenyeji wa Mangochi mwenye asili ya Uyao Alhaj Bakili Muluzi
ambapo baadaye Rais Bingu wa Mutharika ndiye aliyechukua nafasi hiyo hadi sasa.
Nchi ya Malawi
imepata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 ikiwa ni miaka mitatu baada
ya Uhuru wa Tanganyika.
Katika
kuenzi harakati za ukombozi za nchi hiyo baadhi ya wasanii wa nchi hiyo
wametengeneza igizo maarufu linalozungumzia John Chilembwe ambaye ndiye
anayeelezwa kuwa ni mkombozi wa kweli huku baadhi ya waimbaji wakiimba nyimbo
mbalimbali za kuomboleza vifo vya wanaharakati waliotengenezewa ajali na
serikali ya wakati wa Dkt. Kamuzu Banda.
Aidha
vuguvugu la mageuzi wakati wa ukoloni nchini Malawi linaelezwa kuwakimbiza raia
wengi wakiwemo Rais wa Kwanza wa Visiwa vya Zanzibar Abeid Aman Karume,akina
Oscar Kambona,John Chipaka na wengine wengi waliohama nchi hiyo kwa sababu
zinazoelezwa kuwa ni ukandamizaji wa wakoloni.
Post a Comment
Post a Comment