CCM imemtangaza mgombea Ubunge katika Jimbo la
Arumeru Siyoi Sumari aliyepata kura 761 dhidi ya kura 361 alizopata mpinzani
wake wa karibu Bw.William Sarakikya.
Kwa hutua
hiyo Bw.Sumari ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw. Jeremiah
Sumari ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha kuwania
nafasi hiyo dhidi ya vyama vya vingine hususani CHADEMA.
Kwa mujibu
wa Msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Pius Msekwa ni kwamba uchaguzi huo umerudiwa
baada ya uchaguzi wa awali kumkosa mshindi kutokana na wagombea kupata kura
chini ya asilimia 50.
Katika
uchaguzi wa awali Sumari alipata kura 316 na Sarakikya alipata kura 259.
Uchaguzi huo
umefaanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw.Jeremiah Sumari
aliyefariki Januari 19 mwaka huu.
Post a Comment
Post a Comment