VILIO VYATAWA MWILI WA WILLY EDWARD ULIPOWASILI KWAO MUGUMU
Mdogo wa marehemu Willy Edward (kushoto) akilia huku akilakiwa na ndugu yake baada ya mwili wa marehemu Willy Edward kuwasili nyumbani kwao juzi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Willy Edward ukiingizwa ndani baada ya
kuwasili nyumbani kwao Mugumu, wilayani Seerengeti juzi usiku.
Mjane wa marehemu Willy Edward Rehema, akilia kwa uchungu juu ya jeneza
la mumewe baada ya mwili kuwasili nyumbani kwao Mugumu juzi.
Baadhi ya ndugu wa marehemu Willy Edward, wakiangua kilio baada mwili kuwasili nyumbani kwao Mugumu, Serengeti juzi.Baba mkubwa wa marehemu Willy Edward, Emmanuel Ongiri, akilia kwa uchungu huku akiwa amelalia jeneza lenye mwili wa mwanawe ulipowasili nyumbani kwao Mugumu, Serengeti juzi usiku
.
Mmoja wa waombolezaji akisoma habari za kifo cha aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo leo, marehemu Willy Edward wakati wa shughuli za msiba mjini Mugumu, wilayani Serengeti jana.
Mzee Edward Ogunde, baba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akifarijiwa na mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapicha gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania, Anicetus Mwesa nyumbani kwao marehemu, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti jana. Willy anazikwa leo eneo la nyumba yao kjaribu na kaburi la mamake. Katikati ni mdogo wa marehemu, Essey Ogunde.
Mmoja wa waombolezaji Noah Ongiri, akitumbuiza kwa kutumia kipaza sauti alichojitengenezea wakati wa msiba wa mpendwa wao marehemu Willy Edward. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment
Post a Comment