Ads (728x90)




Na, Kibada Kibada – Mpanda, Katavi.
Waziri  Mkuu Mizengo  Pinda amewasili uwanja wa ndenge wa Kashaulili ulioko Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi kwa ajili  ya mapumziko mafupi .
Waziri Mkuu Pinda mara baada ya  kuwasili  Uwanja wa Ndege wa Mjini Mpanda alipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali Mkoani  Katavi  kisha kuelekea kijijini kwake alipozaliwa Kata ya Kibaoni Kijiji cha Kibaoni.
Akiwa nyumbani kwake atapumzika na kusalimiana na wazazi wake pamoja na ndugu na jamaa zake kijijini hapo.na mara baada ya  mapumziko hayo atafanya ziara ya kutembelea wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo mkoani humo.
Mbali ya kutembelea wananchi na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali atakayopangiwa kwa mjibu wa ratiba pia atazindua  bodi mpya ya barabara ya mkoa wa katavi,pamoja na kufungua kikao cha kwanza cha ushauri cha mkoa mpya wa Katavi , pamoja na shughuli nyingine za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzindua umeme unaotumia nguvu ya jua maarufu kwa jina la umeme wa solar.
Baada ya kumaliza ziara yake waziri mkuu  atarejea jijini Dar es salaam.
Katika hatua nyingine mafunzo ya makarani watakaohusika na zoezi la sensa ya watu na makazi yaliyokuwa yakifanyika maeneo mbalimbali mkoani katavi yamemalizika leo kwa kufungwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima.
Akifunga mafunzo hayo mkuu wa Wilaya ya  mpanda ameasaa makarani kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo muhimu la kuhesabu watu ili kupta takwimu sahihi kwa maendeleo ya taifa.
Amesema zoezi la sensa ni muhimu kwa taifa kupata takwimu sahimu ambazo zitasaidia kutumika katika kupanga mipngo ya maendeleo ya taifa , shughuli za tafiti na  kupnga mipango ya sera ya kitaifa kwa kuwa unakuwa na takwimu muhimu na hata kwa upande wa familia ukiwa na takwimu sahihi zinasaidia kuweka mambo yako sawa sawa.
Kwa upande wao wahitimu hao wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa umakini mkubwa kwa kuwa kile walichofundishwa wamekielewa barabara ingawa kumekuwa na kasoro za hapa na pale ambazo zinazungumzika na kurekebishika kuhakikisha zoezi la sensa linafanikiwa vizuri.

Post a Comment

Post a Comment