| Na, Rashid Mkwinda ZIKIWA zimepita siku nne tangu 
watu 11 kufa katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwemo gari la 
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dkt. Mary Mwanjelwa, watu wengine 
20 wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea eneo la Mafiat katikati ya 
Jiji la Mbeya.
 
 Ajali hiyo imehusisha magari mawili aina
 Pick Up Double Cabin Ford Ranger yenye namba za usajili T 189 BLP 
iliyokuwa ikielekea upande Mwaanjelwa ikitokea mjini na Hiace iliyokuwa 
ikielekea TAZARA ambapo magari hayo yalijikuta yakigongana uso kwa uso 
kiasi cha kuwajengea hofu abiria waliokuwemo ndani ya Hiace.
 
 Kwa
 mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba gari aina ya Pick Up 
lilikuwa katika mwendo wa kasi huku Hiace ikikimbilia abiria katika 
kituo kinachofuata na kwamba hakukuwa na tahadhari kati ya madereva wa 
magari.
 | 
Post a Comment