WABABE wa Yanga timu ya wakata Miwa Mtibwa ya Morogoro leo imegonga
mwamba baada ya kupelekeshwa puta na timu ya maafande wa Prison ya Mbeya
na kulazimishwa kutoka suluhu ya bila kufungana katika uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Mpira huo ulianza kwa kasi kwa
kila mmoja kuliandama lango la mwenzie ambapo kinyume na miaka ya nyuma
timu ya Prison imeonekana kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa
nyumbani kwa kulazimisha kutoka suluhu kwa mechi za nyumbani.
Hadi
mapumziko timu hizo zilizokuwa zinachezeshwa na refarii Hashimu
Abdallah kutoka Jijini Dar es salaam zilikuwa zilikuwa hazijaweza kuona
goli la mpinzani wake.
Mbali na michomo kadhaa
iliyokuwa ikielekezwa katika lango la Mtibwa na kuokolewa nma golikipa
Shaaban Kado, Prison nao walikuwa wakihaha kujaribu kuokoa michomo
iliyokuwa ikilengwa kwa golikipa wake Daud Abdalla ambaye kwa muda
mwingi alikuwa akihaha golini akiwapanga walinzi wake Henry Mwalugala,
Laurian Mpalile, Lugano Mwangama na David Mwantika. |
Post a Comment
Post a Comment