Ads (728x90)



MAAJABU YA DUNIA

Stori Na,Rashid Mkwinda

MTOTO wa ajabu amezaliwa katika hospitali ya teule ya Ifisi ya wilaya ya Mbeya huku akiwa hana pua na jicho moja katika paji lake la uso,Kiumbe hicho cha ajabu kilizaliwa juzi majira ya saa 9: alasiri na kuishi kwa takribani saa tisa hadi saa 4:00 usiku kilipoaga dunia.

Wazazi wa kiumbe hicho ni wakazi wa kijiji cha Mwampalala Iwindi nje ya Jiji la Mbeya. 

Inaelezwa kuwa mama wa mtoto huyo ambaye yuko chini ya miaka 18 aliolewa na mumewe Emanuel Mbukwa(24) miaka miwili iliyopita lakini kwa bahati mbaya katika maisha yao binti huyo hajawahi kubahatika kupata ujauzito.

Kwa mujibu wa mama wa kiumbe hicho(jina linahifadhiwa kwa kuwa yuko chini ya miaka 18) ni kwamba katika  miaka hiyo miwili waliyoishi na mumewe hajawahi kupata ujauzito hivyo walifanya jitihada za mitishamba na mumewe ili angalau wapate mtoto.

‘’Tumehangaika sana na mume wangu, hatimaye nikapata ujauzito, nilikuwa nahudhuria kliniki kama kawaida lakini bahati mbaya ndio haya matokeo yake,’’alisema binti huyo mzazi wa kiumbe hicho.

Alisema kuwa alitembea sana kwa waganga wa kienyeji na kula kila aina ya  mitishamba ili apate ujauzito na kwamba ilipofikia wakati wa kujifungua alijifungua mtoto asiye na pua, na mwenye jicho moja katikati ya paji lake la uso.

TAMATI.

Post a Comment

Post a Comment