| 
 
TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” KUHUSIANA NA HALI YA
UHALIFU KWA KIPINDI CHA KUANZIA JANUARI 2012 HADI DESEMBA TAREHE 30/12/2012. 
 
1.0.Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI anatoa shukrani na pongezi za dhati kwa wananchi wa
Mkoa wa Mbeya kutokana na ushirikiano waliouonyesha kwa Jeshi la Polisi katika
jukumu kubwa la kulinda usalama wa maisha na mali zao kwa  kipindi cha mwaka huu 2012 unaotarajia kumalizika leo. Ifuatayo ni taarifa fupi kuhusiana
na  taswira ya hali ya uhalifu katika
Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka 2012. 
1.1.Katika
kipindi cha kuanzia 01.01.2012 hadi
tarehe 30.12.2012  kwa ujumla hali ya uhalifu Mkoa wa Mbeya
ilikuwa shwari. Hata hivyo pamoja na hali hiyo ya  ushwari kulikuwepo na baadhi ya matukio
makubwa ya jinai mathalani  Mauaji,Unyang’anyi wa kutumia
silaha,Unyang’anyi wa kutumia nguvu,Uvunjaji,kubaka, wizi wa Pikipiki wizi wa
mifugo n.k. ambayo yaliweza kushughulikiwa na Jeshi la Polisi kwa mafanikio
makubwa kwani watuhumiwa wameweza kukamatwa na kufikishwa Mahakamani na baadhi
yao kesi zimemalizika na wengine  kesi
zao zinaendelea kusikilizwa zikiwa katika hatua mbalimbali. 
          [a]
TATHMINI YA MAKOSA  YOTE YA JINAI. 
 
Katika kipindi hicho cha
Jan  – Desemba   2012 jumla ya makosa 29,849 yaliripotiwa
katika vituo mbalimbali vya Polisi , wakati kipindi kama hicho mwaka 2011
makosa 25,699 yaliripotiwa, hivyo kuna ongezeko la makosa 4,150  sawa na asilimia 16. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa makosa madogo madogo kama
vile kutumia lugha ya matusi,kutishia,shambulio,wizi n.k. 
         [b] TASWIRA YA HALI YA UHALIFU YA MKOA. 
Katika kipindi hicho cha Jan – Desemba  2012 jumla ya makosa 5,761 ambayo ni kero kwa jamii kati ya hayo makubwa  1,430
 na madogo 4,331 yaliripotiwa , wakati kipindi kama hicho mwaka 2011 makosa 7,550 kati ya hayo  makubwa  1,479  na madogo 
6,071 yaliripotiwa, hivyo
kuna pungufu  la makosa 1,789  sawa na asilimia 23. Hata hivyo upungufu huo wa makosa makubwa unatokana na jitihada
za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali katika
kupambana na uhalifu na  
 
wahalifu hususani kwa makosa
makubwa. [ Tazama kiambatanisho jedwali  A na 
B]                                                                                                     
Hapa chini ni jedwali “A” kuonyesha mchanganuo wa makosa
makubwa  ambayo ni kero kwa jamii
yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012
ikilinganishwa na kipindi kama hichi mwaka 2011.                                                                                                              
JEDWALI  ‘A’ 
 
  | 
S/NO 
 | 
MAKOSA | 
01.01.2012 HADI 
30.11. 2012 | 
01.01. 2011 HADI  
30.12.2011 | 
TOFAUTI | 
ASILIMIA |  
  | 
1 | 
MAUAJI | 
276 | 
354 | 
-78 | 
-22 |  
  | 
2 | 
KUBAKA | 
358 | 
379 | 
-21 | 
-5 |  
  | 
3 | 
UNYANG’ANYI KATIKA
  BARABARA KUU | 
4 | 
14 | 
-10 | 
-71 |  
  | 
4 | 
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA
  SILAHA | 
14 | 
17 | 
-3 | 
-17 |  
  | 
5 | 
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA
  NGUVU | 
165 | 
171 | 
-6 | 
-3 |  
  | 
6 | 
UVUNJAJI | 
266 | 
292 | 
-26 | 
-8 |  
  | 
7 | 
WIZI WA MIFUGO | 
233 | 
196 | 
+37 | 
+18 |  
  | 
8 | 
WIZI WA PIKIPIKI | 
114 | 
56 | 
+58 | 
+103 |  
  | 
9 | 
WIZI | 
4, 860 | 
6,071 | 
-1.211 | 
-19 |  
  | 
 | 
JUMLA | 
5,761 | 
7,550 | 
-  1,789 | 
-23 |  
 
1.2. Pamoja
na kupungua kwa makosa makubwa changamoto bado ipo kwa baadhi ya makosa kama
vile WIZI WA PIKIPIKI na WIZI WA MIFUGO ambayo yameongezeka. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI, anawataka waendesha Pikipiki waendelee kuwa na
umoja katika kudhibiti uhalifu na kutoa taarifa za uhalifu kwa mamlaka
zinazohusika  hasa kwa watu ambao
wanawatilia shaka. 
 
                                                                      
                                            
2.0.TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO NA
JITIHADA  ZA  POLISI         
     
KWA  KUSHIRIKIANA NA WANANCHI  NA WADAU MBALIMBALI. 
 
Katika
kipindi cha kuazia tarehe 01.01.2012
hadi tarehe 30.12.2012 makosa kadhaa
yatokanayo na jitihada za Polisi na wadau wengine yalidhibitiwa  kwa mafanikio makubwa. Hii ni kutokana na
misako,doria na operesheni mbalimbali zilizofanyika.                                                                                                           
Hapa chini ni jedwali  “B” kuonyesha mchanganuo wa makosa  yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana wananchi na wadau mbalimbali ambayo ni kero kwa jamii
yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hichi
mwaka 2011. 
 JEDWALI ‘B’ 
 
  | 
S/NO | 
        MAKOSA | 
01.01.2012
  HADI 30.12.2012 | 
01.01.2011
  HADI 30.12. 2011. | 
TOFAUTI | 
ASILIMIA |  
  | 
                1 | 
WAHAMIAJI HARAMU | 
72 | 
24 | 
+48 | 
+200 |  
  | 
2 | 
KUPATIKANA NA BHANGI  | 
171 | 
148 | 
+23 | 
+15 |  
  | 
  3 | 
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU
  YA MOSHI [GONGO] | 
91 | 
44 | 
+47 | 
+106 |  
  | 
4 | 
KUPATIKANA NA MTAMBO WA
  GONGO | 
12 | 
4 | 
+8 | 
+200 |  
  | 
 5 | 
KUPATIKANA NA SILAHA  | 
24 | 
15 | 
+9 | 
+60 |  
  | 
6 | 
KUPATIKANA NA RISASI | 
10 | 
3 | 
+7 | 
+233 |  
  | 
7 | 
MAGENDO | 
10 | 
4 | 
+6 | 
+150 |  
  | 
8 | 
KUPATIKANA NA MADAWA YA
  KULEVYA. | 
6 | 
- | 
+6 | 
+600 |  
  | 
9 | 
KUPATIKANA NA NYARA ZA
  SERIKALI. | 
22 | 
17 | 
+5 | 
+29 |  
  | 
 | 
JUMLA 
 | 
418 | 
259 | 
+159 | 
+61 |  
                                                                                                
                                         
                                                                                                                                      
Kuongezeka
kwa makosa haya kunatokana na jitihada za dhati za Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi na wadau wengine katika kukabiliana na uhalifu.                                                                                          
2.1
BAADHI YA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA. 
 Katika kipindi cha kuanzia tarehe 01.01.2012 hadi tarehe 30.12.2012 baadhi ya mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na :-                                                                                                                         
·       
Pombe
ya moshi [gongo] yenye ujazo wa lita 787 zilikamatwa pamoja na mitambo 12  ya kutengenezea pombe hiyo.     
·       
Bhangi
yenye uzito wa Kgm 942   na  gram 631 pamoja na shamba moja lenye ukubwa
wa ekari 1 ilikamatwa. 
 
·       
Wahamiaji
haramu  535 wamekamatwa katika mchanganuo
ufuatavyo:- 
Ø Ethiopia   192 
Ø Somalia    298 
Ø Kenya       1 
Ø Malawi   11 
Ø DRC      33 
·       
Silaha
20  zimekamatwa kati ya silaha hizo Gobole
16, SMG 2 na risasi 178, Riffle  1, S/gun
1 na  risasi 12. 
·       
Jumla
ya watuhumiwa  9,581 wamekamatwa kwa
makosa mbalimbali kati yao 5,101 wamefikishwa Mahakamani.  
·       
Magari
11 yaliyokuwa yameibwa yamepatikana. 
·       
Noti
bandia 292 kati ya hizo 197 @ tshs 10,000/= sawa na tshs 1,970,000/= na noti 95
@ tshs 2,000/= sawa na tshs 190,000/= zilikamatwa. 
·       
Madawa
ya kulevya aina ya Cocaine Kgm 3 na gram 979 na Heroine gram 4.5 yalikamatwa. 
·       
Mafuta
ya wizi aina ya Diesel lita 5,855 zilikamatwa. 
·       
Bidhaa
za magendo za aina mbalimbali zenye thamani ya tshs 9,800,000/= zilikamatwa. 
·       
Mifuko
45 ya simenti maalum kwa ajili ya ujenzi  wa barabara ilikamatwa 
·       
Pikipiki
11 zilikamatwa katika matukio mbalimbali 
ya kihalifu.  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
·       
Milipuko
ya aina mbalimbali kwa ajili ya kupasulia miamba /mawe yenye thamani USD
3,600  [tshs 5,760,000/=] iliyoporwa
ilikamatwa ambayo ni :- 
Ø Kubella pc 275 
Ø Detector pc 309 
Ø Cordetex Roll mita
1,750                                                          
 
Ø Led pc 7 
Ø Trunkerline Roll 13.                                                                      
 
                                                                                                            
·       
Kupungua
kwa matukio makubwa ya uhalifu kama inavyoonekana kwenye jedwali “A” 
                                                                
                              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI
ATHUMANI  pamoja na kutoa shukrani
kwa mafanikio hayo, bado anaendelea kutoa rai kwa jamii kulipa ushirikiano wa
karibu Jeshi la Polisi ili kuwafichua wahalifu kwani  uhalifu unarudisha nyuma maendeleo ya mwana
Mbeya mmoja mmoja /familia hadi Mkoa mzima 
na Taifa kwa ujumla.  
3.0
MAKOSA YA USALAMA BARABARANI. 
Makosa
ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani katika kipindi cha mwaka  2012
hususani ya ajali yamepungua  ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2011. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI  anasisitiza kuwa pamoja na upungufu huo wa
matukio ya ajali  bado zipo changamoto
katika kukabiliana na matukio ya ajali Mkoa wa Mbeya ambayo ni pamoja na :-  
§  Mwendo
kasi wa magari /Pikipiki kwa baadhi ya madereva na kutokuwa makini kuzingatia
sheria za usalama barabarani na baadhi ya wananchi kushabikia mwendo kasi.                                                   
                               
§  Ulevi 
§  Kupita
gari lingine bila tahadhali [Overtaking] 
§  Tatizo
la kimiundo mbinu kamamvile milima/maporomoko n.k 
§  Mwendo
kasi [Overspeed] maeneo ya tambarale. 
§  Wananchi/watembea
kwa miguu kutokuwa makini na matumizi ya barabara. 
 
 
 
 
 
 
Hapa chini ni jedwali “C” kuonyesha
mchanganuo wa makosa  ya ukiukwaji wa
sheria za  usalama barabarani
yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hichi
mwaka 2011.                                                              
                                                                                                                       
JEDWALI  ‘C’ 
 
  | 
S/NO | 
        MAKOSA | 
01.01.2012
  HADI 30.12.2012 | 
01.01.2011
  HADI 30.12. 2011. | 
TOFAUTI | 
ASILIMIA |  
  | 
                1 | 
JUMLA YA MAKOSA YOTE YA
  UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI | 
52,716 | 
40,823 | 
+11,893 | 
+29 |  
  | 
2 | 
MATUKIO YA AJALI | 
598 | 
686 | 
- 88 | 
-12 |  
  | 
3 | 
AJALI ZA VIFO | 
246 | 
254 | 
   -8 | 
-3 |  
  | 
4 | 
WATU WALIOKUFA | 
315 | 
320 | 
-5 | 
-1 |  
  | 
 5 | 
AJALI ZA MAJERUHI | 
352 | 
432 | 
-80 | 
-18 |  
  | 
6 | 
WATU WALIOJERUHIWA | 
802 | 
812 | 
-10 | 
-1 |  
  | 
7. | 
TOZO
  [NOTIFICATION] 
KUTOKA KWA WAKOSAJI
  MBALIMBALI. 
 | 
1,250,790,000/= | 
802,130,000/= | 
+448,660,000/= | 
+55 |  
   
4.0
HALI YA KISIASA / MIGOGORO YA KIJAMII NA DINI. 
4.1
Hali ya kisiasa, Inaendelea vizuri ,vyama vya siasa Mkoani
Mbeya ambavyo ni pamoja na  CCM,CHADEMA,CUF,TLP na NCCR- MAGEUZI, vimeendelea kufanya
harakati zake kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya hadhara kwa usalama. Hata
hivyo matukio kadhaa ya uvunjifu wa amani yaliripotiwa kutokea katika Kata za
Kiwira Wilaya ya Rungwe na  Mpapa na
Kamsamba  Wilayani Momba wakati wa
kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani na Mwenyekiti wa
Serikali ya Kijiji , matukio hayo yaliweza kudhibitiwa kwa watuhumiwa
kadhaa  kukamatwa na kufikishwa
Mahakamani, kesi zao zinaendelea.      
 
 
                                                                                                                     
4.2.
MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI.    
Katika
kipindi hicho hakuna tukio kubwa  lililoripotiwa
kutokea. 
4.3
MASUALA YA IMANI ZA KIDINI. 
Katika kipindi hicho hakuna
tukio la uvunjifu wa amani lililohusiana na migogoro ya imani za kidini
lililiripotiwa kutokea.                             
        CHANGAMOTO. 
Miongoni
mwa changamoto zilizojitokeza kwa kipindi hiki ni pamoja na :-..     
ü Baadhi ya wananchi kuendelea
kuficha wahalifu na uhalifu katika maeneo yao na kushindwa kutoa ushirikiano
kwa Jeshi la Polisi. 
ü Bado baadhi ya
wananchama wa vyama/ viongozi wa siasa hawajaona umuhimu wa kutii sheria wao wenyewe
na ama kuendelea kutoa maneno ya kuwagawa wana Mbeya. 
                                               
5.0 HITIMISHO
/ WITO WA KAMANDA. 
§  Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limejitahidi kudumisha utulivu na amani katika kipindi
chote cha mwaka 2012 ikiwa ni pamoja
na kudhibiti uvunjifu wa amani uliotaka kujitokeza kutokana na migogoro ya
kijamii katika baadhi ya maeneo kama vile Vijiji vya Ntokela na Kiwira Wilaya
ya Rungwe,Tunduma na  Kamsamba Wilaya ya
Momba na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Kamishna msaidizi wa Polisi Diwani Athumani anatoa wito kwa wakazi/wana Mbeya  kwa mwaka ujao wa 2013 :- 
§  Kuendelea
kutoa /kulipa ushirikiano wa karibu  Jeshi la Polisi katika kufichua na kupambana
na uhalifu na wahalifu Mkoa wa Mbeya ili kuhakikisha uhalifu unazidi kupungua
kama sio kumalizika kabisa na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kujipanga
kuhakikisha Mkoa unakuwa shwari na wananchi wanaendelea kufanya shughuri zao za
kujitafutia  maendeleo kwa amani,utulivu
na usalama na pia inashiriki katika ulinzi na usalama wao wenyewe na mali zao.  
§  Wananchi
kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi katika matatizo                       yanayowakabili badala yake watafute ufumbuzi kwa
njia ya mazungumzo   /utaratibu
unaokubalika kisheria  kupitia mamlaka
husika yakiwemo  matatizo ya kijamii.  
 
 
 
§  Kamanda
ameeleza kuwa vitendo vya  kufunga barabara
na kuchoma matairi ni uharibifu wa miundo mbinu inayopelekea hasara kubwa kwa
Taifa na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara. Aidha vitendo hivyo
vimekuwa vikisababisha  kuwa na watu
ambao wameonyesha kutokuwa na nia njema ikiwa ni pamoja na kufanya uporaji                                                                    
                              
§  Viongozi
wote wa dini/siasa/jamii n.k waendelee  kuwafanya wana Mbeya kuwa wamoja badala ya
kuwagawa bila kuathiri shughuli zao ziwe za kidini/kisiasa/kijamii wakikumbuka
kuwa umoja ndio chachu kubwa ya maendeleo.                                                                                    
                                
§  Aidha  anawatakia wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya  na watanzania kheri ya mwaka   mpya 2013.
Aidha Kamanda anasisitiza  kusherehekea
kwa amani na utulivu pasipo kuhusisha vitendo vya vurugu,uchomaji moto matairi
, kufunga barabara na uendeshaji mbovu wa vyombo vya moto kwani ni kinyume cha
sheria. 
 
Signed By 
[ DIWANI ATHUMANI – ACP ] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
 
                                                      
                                               
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 | 
Post a Comment
Post a Comment