MFANYABIASHARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI
Mfanyabiashara mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya aliyefahamika kwa
jina la Cosmas Kunzugala(60) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia jana
nyumbani kwake Iyela Jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa
vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Diwani Athumani
alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa na na watu hao majira ya saa 5:40
usiku.
Kamanda Diwani amesema kuwa mbinu iliyotumiwa na wauaji hao
ni kumgongea mlango mfanyabiashara huyo ambapo mara alipotoka kufungua mlango
alipigwa risasi kifuani na mkono wa kushoto na kufa papo hapo.
Amesema kuwa mara baada ya mauaji hayo wauaji hao
walitokomea kusikojulikana ambapo hata hivyo alisema kuwa hakuna mali
yoyote iliyochukuliwa ambapo mara baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuingia ndani.
Aidha Kamanda Diwani amesema kuwa katika eneo la tukio
iliokotwa goroli moja ambayo hutumika katika bunduki aina ya Shirt Gun ambapo
jeshi la polisi linachunguza chanzo cha
mauaji hayo na mwili wa marehemu umehofadhiwa katika hospitali ya rufaa ya
Mbeya.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI |
Post a Comment
Post a Comment