VIONGOZI
waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA pamoja na wanachama 15
wa chama hicho wanatarajia kujiunga na Chama Cha NCCR Mageuzi kesho katika
ukumbi wa Hotel ya Double J jijini Mbeya.
Kwa mujibu
wa taarifa za chama hicho zilizotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya
mkononi kwa wanahabari imedaiwa kuwa viongozi hao wa CHADEMA watakutana na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda
Juju ambaye atamwakilisha, mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho James Mbatia.
Juju ambaye
tayari amewasili mkoani Mbeya kwa shughuli hiyo maalum anatarajia kuwapokea
viongozi hao wa CHADEMA ikiwa ni hatua za awali zinazodaiwa kukisambaratisha
CHADEMA.
Hivi karibuni
aliyewahi kuwa Katibu wa Mkoa wa CHADEMA Eddo Makata alitangaza kujiunga na
NCCR-Mageuzi baada ya kujiuzulu kutoka CHADEMA ambapo hata hivyo viongozi wa
CHADEMA walidai kuwa walimtimua uongozi na uanachama.
Wimbi la
mpasuko ndani ya CHADEMA limeanza kuibuka baada ya madai ya kutimuliwa kwa
viongozi na wanachama wa chama hicho akiwemo, Makamu Mwenyekiti Baraza la
Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA)Juliana Shonza na aliyewahi kugombea Ubunge
jimbo la Mbozi Mashariki Mtera Mwampamba.
|
Post a Comment
Post a Comment