Ads (728x90)

MABANGALUU HAYA YAMEJENGWA KWENYE ARDHI OEVU WILAYANI MBOZI, UTOAJI WAKE WA HATI MILIKI UKOJE, WAKUU WA IDARA YA ARDHI KUWAJIBIKA?

HATA HOTELI HII IKO KATIKA ARDHI OEVU SHERIA NI MSUMENO, VIONGOZI WATAAMUA KUTAFUNA JONGOO KWA MENO NA KUONDOA UWEKEZAJI HUU ULUOGHARIMU MAMILIO YA FEDHA?

PAMOJA NA KUWEPO KWA ILANI HII YA KUTOENDELEA NA UJENZI KATIKA ENEO HILI LA ARDHI OEVU WILAYANI MBOZI, LAKINI BADO UJENZI UNAENDELEA KAMA UNAVYOONEKANA PICHANI, MMILIKI WA NYUMBA HIYO ANA HATI NA RAMANI ALIYOPEWA NA MAOFISA ARDHI, JEE ITABOMOLEWA NANI ATAKAEYFIDIA GHARAMA HII?


UWEKEZAJI HUU UTAIINGIZA HALMASHAURI YA MBOZI GHARAMA YA MAMILIONI YA FEDHA KUTOKANA NA MAJENGO HAYO KUJENGWA KATIKA ARDHI OEVU HUKU MAOFISA ARDHI WAKIHUSIKA KATIKA UGAWAJI WA VIWANJA HIVI.


WANANCHI WA HALI DUNI NAO WAMEKUJA JUU KUKATAA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO AMBAZO ZIMEWEKWA ALAMA YA X ILHALI NYUMBA ZA VIGOGO ZIMEACHWA .


OFISA ARDHI WA WILAYA YA MBOZI  MOSES KIBONA AMEWEKWA KITI MOTO NA WANANCHI NA KUHITAJIWA KUTOA MAELEZO YA KINA JUU YA UTATA WA UGAWAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA ARDHI OEVU WILAYANI MBOZI

NAYE OFISA MTENDAJI WA MAMLAKA YA MJI WA VWAWA HAKUACHWA NA WANANCHI AMBAO WALIMUELEZA KUWA YEYE NI MOJA YA MATATIZO JUU YA UGAWAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA ARDHI OEVU.

WANANCHI WAKIENDELEA KUTOA MSIMAMO JUU YA KUTOKUBALI KUONDOKA KATIKA ENEO WALILOJENGA HUKU WENYE MAJUMBA YA KIFAHARI WAKIACHWA BILA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO





MKUU WA WILAYA YA MBOZI DKT. MICHAEL KADEGHE AKIELEZA MSIMAMO WA SERIKALI KWAMBA NYUMBA ZOTE ZILIZOJENGWA KATIKA ENEO LA ARDHI OEVU ZITAWEKWA ALAMA YA X KWA AJILI YA KUBOMOLEWA BILA KUJALI KWAMBA NYUMBA HIYO INA HADHI YA NAMNA GANI.

























ENEO LA ARDHI OEVU KAMA LINAVYOONEKANA PICHANI HUKU UPANDE MWINGINE UKIWA UMEVAMIWA KWA UJENZI

Post a Comment

Post a Comment