SIKU
CHACHE BAADA YA MALALAMIKO YA MWANAMUZIKI LADY JAY DE DHIDI YA KITUO CHA
RADIO CHA CLAOUDS FM NA MKURUGENZI WAKE RUGEMALILA MUTAHABA HATA KUTANGAZA
HADHARANI KWA KUTOA WOSIA MZITO WA KUMPIGA MARUFUKU RUGE KUTOHUDHURIA MAZISHI
YAKE IWAPO ATAFARIKI DUNIA.
LADY
JAY DEE AU MAARUFU KWA JINA LA BINT MACHOZI AU KOMANDOO KAMA ANAVYOFAHAMIKA
MIONGONI MWA WAPENZI WAKE ALIFIKIA HATUA HIYO BAADA YA MADAI YA KUWEKEA
KAUZIBE JUU YA MAENDELEO YAKE YA KIMUZIKI NA KUTAKA KUUPOTEZA UMAARUFU WAKE.
KATIKA
MAZUNGUMZO YAKE KUPITIA MTANDAO JIDE ALIKARIRIWA AKISEMA KUWA LENGO LA CLOUDS
FM KUMUONA AMEANGUKA NA ANAPOTEA KATIKA RAMANI YA MUZIKI NA KWAMBA UAMUZI
WAKE NI KUKATAA KUBURUZWA NA KUDAI KUWA KINACHOFANYIKA KWA CLOUDS NI KUWA
HAKUNA MSANII AMBAYE ANAWEZAKUFANYA VIZURI BILA CLOUDS FM.
ALISEMA
KUWA UMAARUFU WAKE HAUKUTOKANA NA CLOUDS FM BALI JITIHADA ZAIKE BINAFSI NA
KWAMBA IWAPO WAO WALIMBEBA BASI WALIPASWA KUWABEBA DADA ZAO WALIOZALIWA NAO
TUMBO MOJA ILI WAWEZE KUIMBA NA KUFIKIA UMAARUFU WANAODAI UMETOKANA NA CLOUDS.
‘’KAMA
KWELI WEWE KUSAGA UNAJUA KUBEBA BASI BEBA JIWE LIIMBE LIWE STAR’’ALISEMA
JIDE.
KATIKA
KUONESHA KUWA AMEKERWA ZAIDI JIDE ALINUKULIWA AKISEMA KUWA HATA SIKU AKIFA
CLOUD FM WASIPIGE NYIMBO ZAKE NA WALA KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA KUWA IWAPO
WATAJITOKEZA WATU HAO KATIKA MAZISHI YAKE WAPIGWE MAWE.
MARA
BAADA YA KAULI HIYO RUGE KUPITIA KIPINDI CHA POWER BREAKFAST KINACHORUSHWA NA
CLOUDS FM ALIAMUA KUKATA UKIMYA NA KUELEZEA HALAI HALISI JUU YA MGONGANO HUO.
RUGE ALISEMA KUWA CLOUDS WALIMPA SAPOTI
KUBWA SANA KIMUZIKI IKIWEMO NA KUSAIDIA ALBUM YAKE YA KWANZA YA MACHOZI NA
KWAMBA YEYE NDIYE ALIYEMSHAURI LADY JAY DEE PAMOJA NA BAADHI YA WANAMUZIKI
WENZIE KAMA VILE RAY C NA SOGGY DOGGY KUACHANA NA UTANGAZAJI NA KUJIKITA
ZAIDI KWENYE MUZIKI.
KUHUSU
MALALAMIKO YA KUITANGAZA ZAIDI BENDI YA SKYLIGHT RUGE ALISEMA KUWA BENDI HIYO
SI MALI YA JOSEPH KUSAGA MKURUGENZI WA CLOUDS FM WALA YEYE BALI BENDI HIYO NI
MALI YA SEBASTIAN NDEGE NA KUONGEZA KUWA IWAPO UPO MVUTANO WA BAINA YA
MACHOZI BAND NA SKYLGHT UTAKUWA NI MVUTANO WA KIBIASHARA KWANI BENDI ZOTE
ZINALIPIA MATANGAZO KWENYE RADIO HIYO.
RUGE
ALISISITIZA KUWA RADIO HIYO NI BINAFSI HIVYO INA UAMUZI WAKE BINAFSI WA
KUPIGA NA KUACHA BAADHI YA NYIMBO NA KWAMBA WANAOWAKEJELI WANAPASWA KUKUMBUKA
WALIKOTOKEA KABLA HAWAJAPATA UMAARUFU WALIONAO.
|
Post a Comment
Post a Comment