TIMU ya
Kimondo ya Mbozi Mbeya leo imejihakikishia matumaini ya kucheza ligi daraja la
kwanza baada ya kuichapa timu ya Stendi ya Shinyanga Bao 1-0, bao ambalo
lilipatikana kwa njia ya penalt dakika ya 20.
Bao hilo
lilifungwa na mchezaji Jofrey Mlawa baada ya mchezaji wa timu ya stendi Nelson
Mtambo kufanyiwa madhambi karibu na goli la timu ya Stendi Shinyanga, goli
lililodumu hadi mpira unamalizika.
Mchezo huo
ambao ulikuwa ukichezeshwa na refarii Zayumba Mapunda uligubikwa na rafu za
hapa na pale hali iliyomfanya refarii kumzawadia kadi nyekundu mchezaji wa timu
ya Stendi David Mwita ambaye alimchezea mchezo usio wa
kiungwana mchezaji wa timu ya Kimondo.
Aidha timu
ya Stendi ya Shinyanga imedaiwa kuwachezesha wachezaji wawili mamluki kutoka
timu ya Njombe mji ambao ni John Milenge ambaye katika timu ya Njombe alikuwa
akitumia jina la John Ganga na Tola
Mwangonela.
Mchezo huo
kumtafuta mshindi wa kwanza na wa pili ambaye ataungana na timu za ligi daraja
la kwanza katika msimu ujao,timu hizo zinatarajia kukutana tena huko mjini
Shinyanga katika mechi ya marudiano, mchezo mwingine unazikutanisha timu za
Polisi Jamii ya Bunda na Friends Rangers ya Jijini Dar.
Post a Comment
Post a Comment