MWANAFUNZI ALIYEJILIPUA NA KUFA KWA MADAI YA WIVU WA MAPENZI DODOMA
Taliki
Juma (22) aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) - Dodoma,
amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Aidha, katika
tukio hilo watu wengine wanane waliokuwa karibu na eneo la tukio
walijeruhiwa vibaya.
Kulingana na taarifa ya Jeshi la Polisi
Mkoa wa Dodoma, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika
Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye eneo la tukio ni kuwa Juma
alimwaga mafuta ya petroli kiasi cha lita tano ndani ya saluni ya Irene
Mapunda na kujilipua.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali ni
kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwa mpenzi wake
aliyejulikana kwa jina la Irene, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili.(kwa hisani ya dar24.com)
Post a Comment
Post a Comment