MILIONI 22
ZACHANGANYWA KUIPIGA TAFU KIMONDO
WADAU
wa
soka wilayani Mbozi na Momba juzi jioni walifanya harambee na kiukusanya
jumla ya sh. milini 22 kwa ajili ya kuipiga tafu timu ya Kimondo ambayo
imepanda ligi
kuu ya daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 14.
Harambee
hiyo ambayo pia iliwahusisha viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA)ilifanyika
katika ukumbi wa Shimoni uliopo mjini Vwawa ambapo mbali na michango hiyo wadau
walitaka kuunganisha nguvu ili timu hiyo iweze kufanikiwa kufuzu kucheza ligi
kuu mwakani.
Mwenyekiti wa
chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala alisema kuwa uongozi wa
mkoa wa Mbeya utaendelea kufanya jitihada kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri
ili kuweka historia ya mkoa wa Mbeya kupandisha timu kila mwaka.
Alisema kuwa
mkoa wa Mbeya una wachezaji wengi wenye vipaji ambavyo vikitumiwa vyema mkoa
utarejea katika ramani ya soka kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Katibu wa
chama mpira wa miguu wilaya ya Mbozi, (MBOFA)William Mwamlima alisema kuwa timu
ya Kimondo imekumbana na changamoto nyingi hadi ilipofikia hatua hiyo hivyo
jitihada za ziada zinahitajia kuisaidia timu hiyo ili iweze kushinda na kucheza
ligi kuu.
Alisema kuwa
jumla ya sh. milioni 92 zinahitajika kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo
hivyo, chama cha mpira wa miguu wilaya ya Mbozi kinahitaji msaada wa hali na
mali ili kuiwezesha timu hiyo kufanikiwa.
Timu ya
Kimondo iko katika kundi inayozihusisha timu nane za Burkina Faso,Polisi na
Mkamba Rangers za Morogoro,Majimaji na Mlale JKT za Songea,Lipuli ya Iringa,na
Kurugenzi ya Njombe.
Kwa mujibu
wa ratiba ya ligi hiyo ambayo imetolewa na chama cha Mpira wa miguu nchini TFF
ni kwamba ligi hiyo inatarajia kuanza Septemba 14 na kukamilika Oktoba 27
ambapo timu zitacheza kwa mtindo wa ligi ya nyumbani na ugenini.
Post a Comment
Post a Comment