DIWANI
WA KATA YA KIWIRA ADAIWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI....
Diwani wa Kata ya Kiwira Wilayani
Rungwe, Lawland Mwakalibule leo amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na
mwanafunzi anayesoma katika Shule ya Sekondari Kiwira, kidato cha Tatu.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Binti huyo alitoweka nyumbani kwao tokea jana,
mpaka aliporejea leo asubuhi, wazazi wake walipombana awaeleze wapi alilala
usiku wa leo ndipo aliposema kuwa alilala na Mhe. Diwani Lawland Mwakalibule.
Baada ya kupata maelezo hayo wazazi
wa mwanafunzi huyu walichukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi
cha Kiwira. Polisi walichukua hatua ya kumtafuta diwani Mwakalibule na kumuweka
chini ya ulinzi wakati upelelezi wa tukio hili ukiendelea. Mtuhumiwa kwa sasa
anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Rungwe mjini Tukuyu.
Mpaka mwandishi wetu anatoka katika
kituo cha polisi mjini Tukuyu mtoto wa shule alikuwa amepelekwa hospitali ya
Wilaya ya Rungwe 'Makandana' kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu.
Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule
akiwa katika kituo cha Polisi Kiwira baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya
mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha Nne.
|
Kituo cha Polisi Tukuyu mahali ambako Diwani wa Kata ya Kiwira Lawland Mwakalibule anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wa shule ya Sekondari Kiwira.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Diwani
Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa ambaye
ni Diwani wa kata ya Kiwira anatuhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato
cha Nne shule ya Sekondari Kiwira.
Kamanda
Diwani alisema kuwa wazazi wa binti huyo Rafael Frank(42) na mkewe Suzan
Frank(38) waligundua kutoweka kwa mazizngira ya kutatanisha kwa binti yao mwenye umri wa miaka
18 (jina linahifadhiwa)ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Nne.
Alisema kuwa
mara baada ya wazazi hao kutomwona binti yao chumbani walitoa taarifa kituo cha
polisi cha Kiwira ambapo jitihada za kumsaka binti yao zilifanyika usiku kucha bila
mafanikio ambapo majira ya saa tatu asubuhi alirejea nyumbani ndipo wazazi
walipomuuliza alikokuwa na kusema kuwa alikuwa kwa mtuhumiwa ambaye ni Diwani
wa kata ya Kiwira Laurent Mwakalibule(28).
Binti huyo
alisema kuwa alilala nyumbani kwa mdogo wa mtuhumiwa hadi asubuhi baada ya
kuwasiliana naye kwa njia simu.
§
Post a Comment
Post a Comment