Ads (728x90)























GARI ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T 993 ALK  imeteketea kwa moto ikiwa zimepita siku nne baada ya kununuliwa na mmiliki mpya wa Kipanya hicho aliyejitambulisha kwa jina la Hans Mtawa.
Kwa mujibu wa Mtawa Gari hiyo ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Baraka Mwanjala ilianza kazi siku nne zilizopita na kwamba leo lilikuwa likitokea Tunduma likiendeshwa na Dereva Adama Mponda.
Alisema kuwa alipata taarifa za kuteketea kwa gari hio alipopigiwa simu na dereva wake ambaye alisema kuwa gari hilo lilileta hitilafu lilipokaribia eneo la Makaburini mjini Vwawa.
Naye kondakta wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jina la Gabriel Mtawa alisema kuwa  gari lao lilianzza hitilafu lilipofika kwenye tuta karibu na stendi ya Makaburini ndipo lilipoanza kutoa moshi mbele kwenye dashboard.
Alisema kuwa walipoona moshi unazidi kutanda waliamua kuvunja vioo vya gari na kutokea madirishani.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika Kipanya hicho.

Post a Comment

Post a Comment