Wachezaji wa Mbeya City hujituma na hata kujitoa mhanga ili kupigania ushindi wa timu yao. |
Bango linaloonesha Majigambo ya Mashabiki wa Mbeya City dhidi ya timu zinazoingia Mbeya kucheza na timu hiyo linalosomeka ''UKIINGIA MBEYA HUTOKI'' |
Wachezaji wa timu ya Mbeya City wakiwaelekea mashabiki baada ya mechi kuwashukuru kwa sapoti yao. |
Wachezaji wa Mbeya City wakitoka kupata baraka za mashabiki wao katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. |
Kikosi cha Mbeya City kilichoitoa jasho timu kongwe ya Coastal Union ya Tanga. |
Kikosi cha Mbeya City kilichowachezesha kwata JKT Ruvu mwishoni mwa wiki. |
Kikosi cha JKT Ruvu kilichocheza na Mbeya City mwishoni mwa wiki na kufungwa bao 1-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya. |
Wachezaji wa Timu ya Mbeya City wakifurahia ushindi na kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. |
-Ina uwezo mkubwa kimchezo,nidhamu na kujituma ni sehemu ya mafanikio yao katika ligi Kuu.
Na Rashid Mkwinda
SIRI
ya majigambo na ushindi wa timu ya Mbeya City inayomilikiwa na
Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo imepanda daraja na kucheza Ligi Kuu na
hatimaye kuwa tishio kwa timu zote zinazocheza ligi hiyo nchini imebainika.
Timu
hiyo inayoongozwa na Mwalimu Juma Mwambusi imejichukulia sifa lukuki ambapo
awali ilionekana kana kwamba inacheza kwa nguvu ya soda huku baadhi ya viongozi
wa timu ilizowahi kucheza nazo walwahi kuibeza wakidai kuwa timu hiyo inacheza
kwa sifa haiwezi kufika mbali kisoka.
Kejeli
aina hiyo ziliwahi kutolewa na kocha wa timu ya Coastal Union ya Tanga ...na
Msemaji wa timu ya Yanga Baraka Kizuguto ambapo kocha wa timu ya Coastal Ally
Kidi alisema kuwa majukumu inayopewa timu hiyo ni makubwa kuliko uwezo wake
hivyo haiwezi kufika mbali ilhali msemaji wa timu ya Yanga Baraka Kizuguto
aliisifia timu hiyo kwa kusema kuwa iwapo ikipata maandalizi ya kutosha inaweza
kuwa timu nzuri ijapokuwa inavurugwa na mashabiki wake wanaoshangilia kupita
kiasi na hata kusababisha vurugu.
Matokeo
ya sare ya 1-1 dhidi ya Yanga yalibezwa huku timu hiyo ikikamiwa kwamba
ikicheza nje ya uwanja wa nyumbani inaweza kufungwa magoli mengi kwa kuwa haina
mashabiki, jibu la maswali hayo lilipatikana katika mechi iliyochezwa katika uwanja
wa Taifa dhidi ya Timu ya Simba ambapo iliilazimisha sare ya mabao 2-2 timu
hiyo kongwe na kuwaacha midomo wazi mashabiki lukuki waliofurika katika uwanja
wa Taifa juu ya uwezo wa timu hiyo changa na ngeni katika ligi Kuu.
Kinachoonekana
katika timu hiyo ni uwezo wao wa kutumia vyema mafundisho ya kocha wa timu yao
Juma Mwambusi sanjari na kujituma kwa wachezaji hao wakiiamini mashabiki
ni sehemu ya ushindi wa timu wao.
Pamoja
na mashabiki wa timu ya Mbeya City kufanya vitendo vilivyowaudhi timu ya Yanga
walipokuwa Jijini Mbeya kwa kuvunja kioo cha Basi lao na hata kumjeruhi dereva
wa gari hilo,waliweza kuwateka mashabiki wa timu ya Yanga katika uwanja wa
Taifa pale wachezaji hao waliposhikana mikono na kwenda upande wa jukwaa la
mashabiki wa Yanga na kuonesha dalili za kuomba radhi kufuatia tukio
lililotokea mkoani Mbeya.
Kitendo
hicho kiliamsha hisia kali za uungwana zilizofanywa na vijana hao chipukizi na
hata kuonesha kuwa ni vijana wenye displin katika mchezo na kwamba kilichotokea
Mbeya hakikukusudiwa na wachezaji hao bali ni cha wahuni wachache waliotumia
fursa hiyo kutaka kuwavurugia mustakabali wao katika ligi kuu.
Mbeya
City ambayo kwa sasa iko nafasi ya pili nyuma ya Azama FC ikiwa na pointi 20
imeendelea kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kujitahidi kushinda katika
kila mechi inayocheza nyumbani na kuendelea kuwapa raha mashabiki wake wa mkoa
wa Mbeya waliotokea kuipenda na kuiunga mkono timu hiyo kwa hali na mali.
Kila
timu iko na siri yake ya ushindi, ushindi wa timu unatokana na uwezo mkubwa wa
kujituma kwa wachezaji hao kuanzia kipindi cha kwanza hadi kipindi cha mwisho
bila kuchoka, nidhamu katika mchezo na mapenzi waliyonayo miongoni mwao na
hata kukubali kukosolewa pale wanapoonekana wanakosea.
Kikubwa
zaidi ambacho kimeonekana kuwavutia wapenzi na mashabiki wengi wa mkoa wa Mbeya
ni desturi yao ya kuwakubali mashabiki wao ambapo wameweza kuiteka hadhira ya
kila mpenzi wa mpira wa miguu Jijini Mbeya, kabla ya kuanza kwa mchezo
wachezaji hao kwa pamoja hujikusanya na kuwaelekea mashabiki wake na kuwapungia
mkono na kuomba baraka zao na hata wanapomaliza mchezo hufanya vivyo hivyo
ambapo nderemo vifijo na vigelegele huendelea kuanzia mwanzo wa mechi hadi
kipyenga cha mwisho kinapopigwa na mwamuzi wa mechi hiyo.
Kikosi
cha timu ya Mbeya City kinaundwa na David Burhani, John Kabanda,Hamad Kibopile,
Yusuf Abdallah,Deogratius Julius,Antony Matogolo,Deus Kaseke,Steven
Mazanda,Paul Nonga, Jeremiah John,Francis Castor, Jofrey Jackkson,Baraka Haule,
Richard Brown, Yohana Moris, Mwagane Yeya, Richard Peter na Peter Mapunda
wakiwa chini ya Mwalimu Juma Mwambusi na msaidizi wake Maka Mwalwisi.
Post a Comment
Post a Comment