Wanafamilia wakibeba mwili wa marehemu Kassim Mboya ambao ulikutwa na pipi 65 zilizosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya |
Mwili wa Kassim Mboya ambao ulikutwa na dawa za kulevya tumboni( Picha zote kwa Hisani ya Mbeya Yetu) |
NYONGEZA YA TAARIFA YA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE
18.11. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – UTAMBUZI WA
MADAWA YA KULEVYA YALIYOPATIKANA
KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.
KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAID MBOYA.
·
MNAMO
TAREHE 15.11.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DSM ULIFANYIKA
UCHUNGUZI WA KITAALAM KUHUSIANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA
YALIYOKUTWA KATIKA MWILI WA MAREHEMU KASSIM
S/O SAID MBOYA.
·
MADAWA
HAYO YALIPOPIMWA AWALI YAKIWA KATIKA MUUNDO WA PIPI ZIPATAZO 65 NA MOJA IKIWA IMEPASUKA ZILIZOVINGIRISHWA
KWA KUTUMIA NYLON MAALUM YALIKUWA NA
UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140. HATA
HIVYO KATIKA UCHUNGUZI HUO MADAWA HAYO YALIBAINIKA KUWA NA UZITO WA GRAM 972. 85 IKIWA NI BAADA YA KUYATOA MADAWA HAYO KATIKA NYLON MAALUM HIVYO UZITO WA NYLON MAALUM PEKEE NI GRAM 167.15 NA YALIBAINIKA KUWA NI AINA YA HEROINE.
§
AWALI
MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA
SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA
MBEYA. KASSIM S/O SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
§
MAREHEMU
ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM
KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA
KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA
AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA
JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD
MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA
MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§
BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI
KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA
TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI
MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA GARI
HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI
KUDHOOFIKA. WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU
ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA
WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU.
HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU
ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 TUMBONI.
§
MNAMO
TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA SAA
14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA
KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI
MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAIDI MBOYA
NDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA
MAREHEMU AITWAE SAID S/O ATHUMANI
MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM
NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN S/O SAID MBOYA, MIAKA 28,
MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA MOHAMED
ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM. BAADA YA UTAMBUZI NDUGU
HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA ALIKUWA
ANAITWA KASSIM S/O SAIDI MBOYA,
MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.
§
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU
KAZI YA TAIFA.
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment