Baadhi ya waendesha Bodaboda wakiwa wamevaa Helmet zilizoziba masikio ambazo zimelalamikiwa kuwa zimekuwa chanzo cha ajali kutokana na waendesha bodaboda hao kutosikia honi za magari. |
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya APEC iliyoandaa mafunzo kwa waendesha Bodaboda wa mikoa 6 nchini. |
Waendesha bodaboda wakiserebuka katika maadhimisho ya siku ya boda boda nchini |
Baadhi ya viongozi wa chama na serikali wilayani Mbozi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Boda boda nchini yaliyofanyika mjini Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya. |
Baadhi ya waendesha Boda boda waliopata mafunzo wakiwa katika maadhimisho ya siku. |
Na Ripota Wetu, Mbozi
WAENDESHA
boda boda nchini wamedai kuwa kofia ngumu zinazoingizwa nchini kwa ajili ya
watumiaji hazina ubora kutokana na kuziba masikio na hivyo kuwafanya watumiaji
kutosikia honi za magari wanapokuwa barabarani na hivyo kuchangia ajali.
Imeelezwa
kuwa kofia hizo maarufu kwa jina la ‘Helmet’ zimekuwa chanzo cha ajali za
barabarani badala ya kuzuia kutokana na kuzibwa masikioni na kwamba ili
kupunguza ajali kofia hizo ziboreshwe ili ziwasaidie waendesha bodaboda.
Akizungumza
wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Boda boda katika kilele cha mafunzo
kwa waendesha bodaboda nchini yaliyofanyika Kitaifa katika wilaya ya Mbozi
mkoani Mbeya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kupunguza Umaskini na majanga na
kuhifandhi Mazingira APEC Bw. Respicius Timanywa alisema kofia za waendesha boda boda hazina Viwango.
Alisema
mazingira ya uendeshaji wa Boda boda yanataka usikivu na umakini kwa kusikiliza
honi za magari na kwamba iwapo zitaendelea kuingizwa kofia zinazoziba masikio
kuna hatari ya ongezeko la ajali nyingi za Pikipiki nchini.
Kwa upande
wake Waziri wa Uchuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo aliwatahadharisha waendesha Piki piki nchini kuzingatia sheria
za usalama wa barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi wanaotokana na
uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani.
Dkt
Mwakyembe alisema kuwa takwimu za vifo na ajali za waendesha boda boda zimekuwa
zikiongezeka ambapo kwa mwaka 2012 kati ya ajali 127 watu 66 walipoteza
maisha kwa nchi nzima ambapo katika mkoa
wa Mbeya kati ya ajali 77 waliopoteza maisha ni watu 37.
Aidha Dkt
Mwakyembe alisema kuwa serikali itapitia kwa kina kero zinazosababisha
ucheleweshaji wa leseni kwa waendesha bodaboda ikiwa ni pamoja na kufuatilia
kwa kina matatizo yatokanayo na ushuru unaotozwa na Halmashauri za Wilaya
ambazo zimekuwa kero kwa waendesha bodaboda.
‘’Mkiona
kuna ushuru usiofaa nijulisheni, zipo kodi zingine za maonezi kwa wananchi
tutazifuatilia ili kuondoa kero hizo,’’alisema Dkt. Mwakyembe.
Alisema ushuru
wote unaosababisha kero kwa wananchi utaangaliwa upya kwa nia ya kuisaidia
jamii itekeleze wajibu wake bila kikwazo chochote cha utendaji katika kukuza
uchumi wan chi.
Kadhalika Dkt.
Mwakyembe aliitaka mamlaka ya Mapato kutochelewesha leseni kwa waendesha
Bodaboda ili kupunguza msururu unaosababisha waendesha boda boda kuchelewa
kupata leseni.
Kwa upande
wake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw.Barakael Masaki alisema kuwa
kumekuwa na ongezeko la ajali kwa mkoa wa Mbeya kati ya Januari hadi Novemba
2013 ambapo jumla ya watu 66 walipoteza maisha na watu 96 walijeruhiwa.
Maadhimisho
hayo ya mafunzo ya waendesha boda boda nchini yamehusisha jumla ya waendesha
bodaboda 30,000 ambapo kati yao kuna wanawake 2600 kutoka mikoa 6 ya Dar es
salaam,Tanga,Morogoro,Simiyu,Shinyanga,Ruvuma na Mbeya.
Post a Comment
Post a Comment