Ads (728x90)

Taarifa zilizosambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na ujumbe mfupi wa simu za mkononi zimeeleza kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa ameanguka ghafla wakati akitoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele alipokuwa anajiandaa kwa ziara ya kutembelea wilaya hiyo.
Inaelezwa kuwa Tuppa alipotoka ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime Henjewele alikuwa akitaka kuingia katika gari lake ili aanze ziara ndipo alipoanguka chini na kuanza kutoa povu, amekimbizwa katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu...taarifa zaidi zitawajia.

Post a Comment

Post a Comment