Ads (728x90)

Mwenyekiti wa Shirika la Without Mother Organization Chriss Zacharia akimkabidhi mafuta ya ngozi Katibu wa Chama Cha Maalbino mkoa wa Mbeya William Simwali.
 
Chriss Zacharia akiwa na viongozi wa Bez Mamy kutoka Jamhuri ya Czech


Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Jamhuri ya Czech Bez mamy na  Club 75 kupitia shirika lao dada la mkoani Mbeya Without Mother Organization wameamua kutoa misaada kwa watu wenye ulemavu wa ngozi  hasa wanafunzi kwa kuwapatia misaada ya mafuta yanayokinga ngozi zao na mionzi ya jua.
 
Mwenyekiti wa shirika la without Mother na Mratibu wa Miradi wa shirika la Bez Mamy Bw Chris Zacharia alisema wameamua kutoa misaada hiyo ili kuwawezesha watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao wanavaa sare za mikono mifupi na kaptula kuhudhuria masomo bila kuogopa mionzi ya jua hasa kuanzia mwezi mei hadi oktoba
 
''Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanashindwa kuhudhuria masomo vizuri wakati wa jua kali kwa kuwa wanaogopa jua na hivyo kushuka kitaaluma na kukosa haki sawa kielimu kama watoto wengine na hivyo kutokuwa na fursa za ajira,'' alisema Zacharia.
 
Mafuta hayo ambayo yanapatika hapa nchini kwa bei kuanzia shilingi 30,000 hadi 80,000 kwa chupa yanatolewa bure na shirika la without mother kwa hisani wa watu wa Jamhuri ya Czech kupitia Bez mamy na Club 75
 
Pamoja na msaada huo kwa albino Without Mother na Bez mamy pia wanatoa misaada ya ujenzi na ukarabati wa madarasa, vitabu vya kiada na madawati katika shule ya msingi Galula wilaya ya Chunya, Shule za msingi Kisa na Ilenge wilaya ya Rungwe, shule za msingi Mahango na Simike wilaya ya Mbarali pamoja na ujenzi wa kituo cha watoto yatima katika kijiji cha mahango wilaya ya Mbarali.(STORI NA PICHA KWA HISANI YA SHIRIKA LA WITHOUT MOTHER ORGANIZATION)

Post a Comment

Post a Comment