Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini John Mwambigija akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hotel ya Mbeya Peak leo asubuhi. |
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Esther Mpwiniza akifafanua jambo katika kikao na waandishi wa habari leo asubuhi |
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mbeya mjini kimedai kuhujumiwa na chama kipya
cha ACT kwa kutumia jina la chama hicho kujitangaza kwa wananchi na kupora
wanachama wake.
Akizungumza
katika kikao na waandishi wa Habari jana katika Ukumbi wa Hotel ya Mbeya Peak
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini John Mwambigija alisema kuwa ACT kimekuwa
kikifanya mikutano ya ndani huku kikijitambulisha kwa majina ya wajumbe wa
Kitaifa wa chama hicho.
Alisema
kuwa hawazikubali mbinu zinazotumiwa na
chama hicho na kuwa kitachukua hatua (hakuzitaja) iwapo kitaendelea
kujitambulisha kwa wananchi kuwa wao ni sehemu ya CHADEMA.
‘’Wameitisha
vikao Ukumbi wa Kiwira Motel, wamejitambulisha kuwa ni wajumbe wa Kitaifa
kutoka CHADEMA, sisi hatuwatambui, lengo lao ni kutuvuruga, hatuwezi kukubali
tutachukua hatua dhidi yao,’’alisema Mwambigija.
Aliffafanua
kuwa taarifa zinazotolewa na viongozi wa chama hicho kuwa ndani ya CHADEMA kuna
ufujaji wa fedha ni za uzushi na kuwa matumizi yote ya fedha za chama hicho
yanaainishwa katika vikao vya utelekezaji kabla ya kupangiwa matumizi yake.
‘’Tuna vikao
vya kupanga matumizi katika chaguzi mbalimbali,hata matumizi ya Helkopta
tunapitisha kwenye vikao na tunakubaliana wajumbe wote wa mkutano, hao
wanaohoji matumizi ya Chopa sisi hatuwatambui,’’alisema Mwambigija ambaye pia
ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Taifa wa chama hicho.
Katika hatua
nyingine chama hicho kimesema kinajiandaa kwa uchaguzi mdogo wa kata ya
Mwasanga Ntembela ambapo watamsimamisha mgombea atakayewakilisha vyama vitatu
vinavyoungana katika Umoja ya Katiba ya Wananchi(UKAWA)
Akizungumzia
uchaguzi huo Katibu Mwenezi wa chama hicho Mbeya mjini Baraka Mwakyabula
alisema kuwa wamekubaliana kwa pamoja na vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF kuwa
mgombea atakayesimama ataungwa mkono na vyama vyote.
Mkutano huo pia uliwahusisha viongozi wa chama
hicho akiwemo Katibu wa Wilaya,Christopher Mwamsiku,Mwenyekiti wa BAWACHA Esther
Mpwiniza,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wilaya Saada Atiki, Kiongozi kamati ya
ulinzi Jamal Juma na Mtunza hazina wa wilaya William Luvanda
Post a Comment
Post a Comment