TUJIKUMBUSHE OCTOBA,2002
Na Rashid
Mkwinda, Mbeya
JESHI la
Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wakiwa na milipuko 675 aina ya baruti na waya mbili wakiziingiza nchinini
kupitia njia za panya katika mji mdogo wa Tunduma uliopo mpakani mwa Tanzania
na Zambia.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mbeya Said Mwema aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Muziki
Michael(32) na Shungu Mponzi(23 raia wa Tanzania ambao walizifunika baruti hizo
na vitenge zikiwa ndani ya sanduku.
Kamanda Mwema
alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Polisi waliokuwa Doria Septemba 29
mwaka huumajira ya saa 1:15 usiku wakiwa na baruti hizo ambapo baada ya
kuhojiwa ilibainika kuwa hawakuwa na kibali cha kuingiza nchini.
Alisema
ilibainika kuwa watuhumiwa hao waliingiza milipuko hiyo kwa nia ya kuwapelekea
wavuvi na wachimba madini huko wilayani Chunya, Watuhumiwa hao wamefikishwa
mahakamani na kusomewa mashtaka wamepelekwa rumande baada ya kukosa dhamana.
Katika tukio
jingine mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Chalangwa wilayani Chunya aliyefahamika
kwa jina la Hans Chapa(70) amefariki dunia akiwa ndani ya nyumba baada ya
nyumba yake kuteketea kwa moto.
Kamanda
Mwema alisema kua tukio hilo lilitokea Octoba 10,2002 majira yab saa 1:00 usiku
baada ya nyumba aliyokuwa akiishi marehemu kushika moto uliowashwa ndani
kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma nyakati za usiku.
Kamanda
Mwema amewaonya wananchi kuwa na tahadhari juu ya matumizi ya moto na kutoacha
moto nyakati za usiku ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Post a Comment
Post a Comment