Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni mwenyeji wa Mpanda ambako wanafunzi wanakosa masomo kwa kukosa maji akizindua wiki ya Maji Mjini Dodoma |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa |
Na Kibada wa Kibada -Katavi
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Mpanda Ndogo iliyopo katika Halmashauri ya Mpanda wilayani Mpanda mkoani Katavi wamelazimika kusafiri umbali wa km 2 kufuata maji yam to kwa ajili ya matumizimbalimbali shuleni hapo.
Wakizungumzia hali hiyo hivi
karibuni mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso aliyefanya
ziara shuleni hapo baadhi ya walimu wa shule hiyo walisemaa moja ya tatizo
linaloikabili shule hiyo ni tatizo sugu la Maji safi na salama.
‘’Tunakabiliwa na tatizo la maji
safi na salama, wanafunzi hulazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata
maji mtoni,’’alisema Rashid Msyete Mkuu wa shule hiyo.
Msyete alisema kuwa mbali na ukosefu
wa maji shule hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi
ikiwa ni pamoja na tatizo la utoro kwa baadhi ya wanafunzi na kukosekana kwa
mlezi wa wanafunzi wa kike wanaokaa Bweni.
Alisema tatizo hilo la maji
limewasababisha kuvunja baadhi ya vipindi kwa ajili ya kusaka maji na hivyo
kusababisha kudorora kwa taaluma kwa wanafunzi hao kwa kuwa muda mrefu wanakuwa
nje ya masomo wakisaka maji.
Kutokana na kuwepo kwa changamoto
hiyo Walimu wa shule hiyo walimwomba Mbunge wao kusaidia kwa namna moja ama
nyingine katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo sugu ambalo mbali na kusababisha
kudorora kwa elimu linachngia utoro shuleni.
Kwa upande wake Mbunge Kakoso aliagiza
Kamati ya Maendeleo ya Kata(KAMAKA) kuketi ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya
kuangalia uwezekano wa mfuko wa jimbo kusaidia katika uchimbaji wa kisima
shuleni hapo kwa nia ya kuondoa kero hiyo.
Post a Comment
Post a Comment