ANSWAR SUNNA WAWAPINGA BOKO HARAM, AL-SHABABI
Ustadhi Ibrahimu Mkate akizungumza katika Ibada ya Swala ya Idd El Fitri kwenye Viwanja vya Kiwanja Ngoma Sokomatola Jijini Mbeya leo asubuhi. |
Ustadhi Ibrahim Mkate akisisitiza jambo wakati wa ibada ya swala ya Id el Fitri leo asubuhi. |
JUMUIYA ya
waislamu wa Answar Sunna mkoani Mbeya wamesema kitendo cha mauaji na utekaji nyara
kinachofanywa na makundi ya Boko Haram na Alqaida ni uovu unaopaswa kupingwa na
waislamu kote duniani kwa kuwa si mafundisho ya dini hiyo.
Akizungumza
wakati wa ibada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani jijini Mbeya Kiongozi
wa Kiislamu ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha King Saud
kilichopo Riyadhi nchini Saudi Arabia,
Ustadh Ibrahimu Mkate alisema watu hao wanapaswa kuuawa kutokana na kupingana na mafundisho ya Uislamu.
Alisema
kinachofanywa na watu hao kinapingana na dini ya Kiislamu hivyo waislamu
wanapaswa kuungana kupinga vitendo hivyo ili kuunusuru Uislamu na waislamu
duniani.
‘’Hii si mila ya dini ya Kiislamu inayohubiri
amani na upendo, hawa wanaowaua watu wasio na hatia, mafundisho haya wanayatoa
wapi,wanavaa mabomu na kujilipua na kuwaua watu wasio na hatia, akina mama,
wazee na watoto, wao ndio wanaopaswa kuuliwa kwa kuudhalilisha Uislamu,’’alisema Ustadh Mkate.
Aliwakana
watu hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijivika jina la Kiislamu na kufanya
mambo yanayoshabihiana na dini ya kiislamu kwa kuwaita kuwa ni makafiri ambao
wanaupinga Uislamu.
‘’Hawa ni maadui wa Uislamu, uislamu
unafundisha Amani na Upendo, wanatuchafua waislamu, sisi hatufundishi kuuana
bila hatia, zipo sheria
zinazotanabahisha nani wa kuuliwa kwa wakati gani na kwa sababu gani,
Aliendelea
kusema kuwa makundi ya Alshabab, Boko
haram, Alqaida ni makundi yasiyofaa
katika Uislamu na kwamba kitendo chao cha kuvaa mabomu na kujilipua ni ukafiri
ambao hauendani na mafundisho ya Uislamu.
Alibainisha kwa kusema kuwa
hiyo si Jihadi kama inavyotafsiriwa bali ni ukatili na unyama unaofanywa na
maadui wa Uislamu ili kuuchafua na kuwa mafundisho ya Muhammad (SAW) kwa
waislamu yalikuwa ni kuingia vitani kupigania dini yao kwa haki dhidi ya wale
wanaowapinga na kuwaua bila haki na sio kuua wasiokuwa na hatia.
‘’Hakuna
Sheria ya kujilipua mabomu kwa waislamu, hiyo sio Jihadi iliyosemwa, huo ni
Ukafiri na wanaofanya hivyo ni Makafiri sio waislamu,’’ alisema.
Post a Comment
Post a Comment