Mahindi ni zao Kuu la Chakula kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambalo likilimwa kwa kuzingatia mbegu bora na mbolea linaweza kumsaidia mkulima akazalsha kwa tija. |
Shamba Darasa |
Shamba darasa katika banda la TAHA |
Banda la maonesho ya mazao ya mbogamboga na maua la TAHA |
Baadhi ya wadau wa kilimo wakiwa katika Banda la MAONESHO la Mbozi |
Baadhi ya bidhaa za mazao ya Kilimo na biashara katika banda la Halmashauri ya Mbozi |
Mwakibete Kasilati Meneja Uwanja wa Maonesho ya Kilimo Nane Nane akifafanua jambo kwenye majumuisho ya siku ya tano ya maonesho ya Kilimo |
Dkt. Fumbuka Mwakilembe Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti Mifugo (TALIRI UYOLE) |
Zao la mahindni ni moja ya bidhaa za chakula zinazozalishwa katika mikoaa ya Nyanda za Juu Kusini |
Respich Maengo Kaimu Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Rukwa, |
Maonesho ya
Kilimo Nane Nane leo yamefikia siku yake ya
nne tangu kuzinduliwa kwake
Agosti 2 naWaziri Mkuu Mizengo Pinda huku kukiwa bado kuna changamoto
mbalimbali zinazowakuta wakulima mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Mikoa sita
ya Nyanda za Juu Kusini ndiyo mwenyeji wa maonesho haya huku Mkoa wa Mbeya
ukiwa ndio msimamizi mkuu wa Uwanja wa maonesho hayo kwa zaidi ya miaka 22.
Mbali na
maudhui halisi ya maonesho hayo kuwa ni kwa ajili ya shamba darasa kwa
wakulima, maonesho hayo yameleta mvuto kwa wafanyabiashara mbalimbali ambao
wamekuwa wakitumia fursa hiyo kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Kauli Mbiu
ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane mwaka huu inasema ‘’Matokeo Makubwa Sasa Kilimo
Ni Biashara, inakwenda sanjari nan uhalisi wa namna ambavyo shughuli mbalimbali
za Kilimo zilivyotekwa na wafanya biashara kwenye mabanda mbalimbali ya
maonesho.
Kaimu Katibu
Tawala Msaidizi mkoa wa Rukwa Respich Maengo alikuwa ni mgeni rasmi kwa siku ya
leo ambaye alitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho, wakati wa majumuisho alitoa
changamoto zake na kusema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya waoneshaji hawajui dhana
ya Kilimo na maonesho hayo.
‘’Nimepita
kwenye mabanda mengi, lakini ajabu waoneshaji hawajui hata kauli mbiu ya mwaka
huu ya maonesho haya inasemaje,?
Maengo kama
walivyo wadau wengine wa Kilimo wanayo dhana hiyo kuwa maonesho hayo yameteka
nyara na wafanyabiashara ambao si wakulima, changamoto kwa waandaaji wa
maonesho hayo TASO kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuhakikisha kuwa maonesho haya
yanakuwa ni ya Kilimo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI UYOLE) Dkt Fumbuka Mwakilembe anasema
kuwa dhana hii ya maonesho inaweza kutoweka iwapo shughuli za biashara zitapewa
kipaumbele badala ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambao ndio walengwa wa maonesho
haya.
Dkt. Mwakilembe anabainisha kuwa katika baadhi
ya nchi shughuli za maonesho ya Kilimo haziingiliwi na maonesho mengine na kuwa
ni vyema taasisi inayosimamia maonesho hayo ikaweka utaratibu wa waoneshaji
halisi wa mambo ya Kilimo.
Mwakibete
Kasilati ni Meneja wa Uwanja wa Nane Nane anasema kuwa changamoto hizo ni
muhimu bali utaratibu wa waoneshaji wengine wasio wakulima kufanya shughuli zao
katika maonesho hayo imekuwepo kulingana na mahitaji ya wananchi wanaotembelea
mabanda ya maonesho.
Anasema kuwa
hata hivyo changamoto hizo ni muhimu kwani zinaibua dhana mpya ya uhalisi na
uwepo wa maonesho hayo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu baina ya mkulima mmoja
na mkulima mwingine kutoka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Post a Comment
Post a Comment