Kikosi cha Mbeya City ambacho kabla ya mechi yake na Ndanda ilikuwa inaongoza kutoka mwisho ikiwa na alama 5. |
Ndanda FC ambao walikuwa wanashikilia nafasi ya pili kutoka mwisho waliopoteza mchezo wake na Mbeya City kwa kufungwa Bao 1-0. |
Mechi inaendelea |
Patashika Uwanjani |
Hatari!!! katika goli la Ndanda FC |
KUTOKA KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE JIJINI MBEYA NI MIMI RASHID MKWINDA WA FASIHI MEDIA INC. |
TIMU ya
Mbeya City ya Jijini hapa imejinasua kutoka mkiani baada ya kuifunga timu ngeni
katika Ligi kuu ya Vodacom kwa Bao 1-0.
Mbeya City
ambayo msimu uliopita ilikuwa tishio kwa timu kubwa baada ya kushika nafasi ya
tatu nyuma ya Azam na Yanga za Jijini Dar es salaam ilianza kuwakatisha tamaa
mashabiki wake kwa kupoteza michezo mingi ya ligi hii.
Hadi inaingia katika mchezo wa leo Mbeya City ilikuwa inaongoza kutoka mwisho huku ikiwa ina akiba ya pointi 5, baada ya ushindi wa leo imejikusanyia jumla ya alama 8.
Mchezo huo
ulianza kwa kasi huku kila timu ikiwa na uchu wa kupata goli ambapo ilikuwa
katika dakika ya nne ya mchezo, Mbeya City ilijipatia goli lililofungwa kwa
njia ya kichwa kupitia kwa mchezaji Deus Kaseke.
Kaseke
alifunga bao hilo baada ya pasi kutoka kwa Themi Felix aliyeupokea mpira kutoka
kwa Paul Nonga.
Golikipa wa
Ndanda alichupa bila mafanikio na mpira ulitinga wavuni.
Hadi
mapumziko Mbeya City ambayo ilikuwa inashangiliwa na mashabiki wachache tofauti
na ilivyokuwa katika mechi zilizopita za ligi hiyo ilikuwa kifua mbele kwa bao
1-0.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Mbeya City ilimuingiza
Mwagane Yeya badala ya Cosmas Fredy na
Ndanda walimuingiza Said Issa badala ya Nassoro Kapama na Idd Kulachi
aliyeingia badala ya Masoud Chile.
Hata hivyo
mabadiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda wala kubadilisha matokeo ya mchezo huo
ingawa kwa upande wa Ndanda United kulionesha kuwa na uhai katika safu ya
ushambuliaji.
Ndanda
walicheza kwa kasi katika kipindi cha pili na kuudhibiti mpira kwa muda mrefu
huku Mbeya City wakionekana kupoteza muda kwa kuanguka anguka mara kwa mara.
Hadi
kipyenga cha mwamuzi wa kike Mary Kapinga kutoka mkoani Ruvuma kinapulizwa
Mbeya City imetoka kifua mbele kwa goli 1 dhidi 0 ya Ndanda United.
Hata hivyo
kocha wa timu ya Ndanda FC Meja Mstaafu Abdul Omar alisema kuwa goli
walilofungwa halikuwa halali kwa kuwa wachezaji wa Mbeya City walikuwa wameotea.
Alisema kuwa
wachezaji wake walicheza kwa kujituma ingawa uwanja ulikuwa ni tatizo kutokana
na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Jijini humo kabla ya mchezo
huo.
Naye Kocha
Juma Mwambusi alisema kuwa ushindi wa timu hiyo ulitarajiwa kutokana na jinsi
walivyojipanga katika mechi zilizopo na kuwa makosa yaliyotokea katika michezo
ya awali yamerekebishwa.
Post a Comment
Post a Comment