TIMU ya Prison ya Mbeya
imeendelea kuutumia vibaya uwanja wake wa nyumbani kwa kulazimisha sare ya Bao
1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani.
Ruvu ndio walikuwa wa kwanza
kuliona lango la Prison mnamo dakika ya 14 ya mchezo baada ya mchezaji aliyevalia
jezi nambari 39 mgongoni Yahya Tumbo
kuwatoka walinzi wa Prison na kufunga bao kwa njia ya Tik Tak.
Prison ambao walionesha kucheza
chini ya kiwango walishambuliwa katika dakika za mwanzo huku wachezaji wake
wakionekana kutoelewana vyema.
Hata hivyo katika dakika ya 30
ya mchezo wachezaji wa Prison walionekana kuamka na kulishambulia lango la Ruvu
ambapo mchezaji Jacob Mwaitalako aliyeingia kipindi cha pili akawainua
mashabiki kwa kusawazisha bao hilo.
Hadi mampumziko timu zote
zilitoka kwa bao kufungana bao 1-1.
Kipindi chja pili hakikuzaa
matunda kwa kila timu ambapo timu zote zilionekana kupaniana huku Prison iliyokuwa
ikielekeza mashambulizi upande wa Kaskazini kukosa magoli mengi ya wazi.
Hadi kipyenga kinapulizwa Prison
1- Ruvu Shooting 1.
Post a Comment