 Mkurugenzi
 wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo  (wa kwanza 
kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari  (hawapo 
pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo  “Tembo 
Supaset 42.5”leo Oktoba 12, 2015 katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. 
Anayemfuatia  ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine 
Langreney pamoja  na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga. Picha zote 
na Cathbert Kajuna.
 Mkurugenzi
 wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo  (wa kwanza 
kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari  (hawapo 
pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo  “Tembo 
Supaset 42.5”leo Oktoba 12, 2015 katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. 
Anayemfuatia  ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine 
Langreney pamoja  na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga. Picha zote 
na Cathbert Kajuna. 
 
Afisa
 Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati) 
akishangilia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge 
Tanzania, Allan Chonjo  (wa kwanza kulia) pamoja na akiwa na Mkurugenzi 
wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga mara baada ya uzinduzi wa chapa mpya ya 
saruji iitwayo  “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es 
Salaam.
 Mkurugenzi
  wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza 
 kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo  
pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo  
Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni  
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na  
Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga.
Afisa
  Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati)  
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  
wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao  
jijini Dar es Salaam. ambapo alisema Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti
  makini uliofanywa na wataalamu wetu  na imetengenezwa mahususi kukidhi
 mahitaji ya soko. 
 Waandishi wa habari pamoja na wageni walioungana katika uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” 
---
Ikiwa
 ni jitihada mahususi kuwapa saruji imara zaidi wakandarasi na 
wafyatuaji matofali Lafarge Tanzania imezindua chapa mpya ya saruji 
iitwayo “Tembo Supaset 42.5” ambayo ni imara na mahususi kwa ufyatuaji 
matofali, zege, majengo makubwa pamoja na miradi mikubwa ya miundombinu 
kama madaraja, barabara na  majukwaa ya michezo.
Akizungumza
 kwenye uzinduzi huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, 
Catherine Langreney alisema kwamba Tembo Supaset 42.5 ni saruji maalum 
iliyobuniwa ili kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya saruji imara na 
inayokauka haraka katika soko la ufyatuaji matofali na zege na ujenzi 
mkubwa “Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na 
wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya 
soko.”alisema.
Akizungumzia
 kuhusu maendeleo katika sekta ya ujenzi Langreney alisema kwamba kwa 
ujumla thamani ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania inakadiriwa kuwa dola 
bilioni. Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 7.8 mwaka 2014 na ni sawa na 
asilimia 8.6 ya pato la taifa ikiwa ni kutokana na ujenzi binafsi, 
usafirishaji na miradi mikubwa ya ujenzi. Tanzania ina idadi ya zaidi ya
 milioni 44 kufikia mwaka 2014 na inatarajiwa kuongezeka sambamba na 
ongezeko la mahitaji ya nyumba na miundombinu.”
Mkurugenzi
 wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo alisema kuwa
 Tembo Supaset ambayo itauzwa kwenye soko la jumla na rejareja ikiwa 
katika ujazo wa kilo 50 ni saruji imara zaidi ikiwa na ubora kuliko 
saruji nyingine zilizopo kwenye soko kutokana na uimara pamoja na bei 
shindani ambazo zimepangwa na itakidhi mahitaji ya watumiaji kama vile:
•    Kuimarika mapema jambo ambalo litawaongezea tija wazalishaji bidhaa zinazotokana na zege
•    Ukaukaji wa haraka jambo litakaloyafanya matofali yaweze kuhamishika haraka na kuongeza tija wazalishaji
•    Mchanganyiko mzuri wa zege na matumizi kidogo ya maji kuimarisha.
Chonjo
 alisema kwamba Tembo Supaset imezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko 
kuwa na saruji imara zaidi huku akitarajia saruji hyo kupanua soko la 
Lafarge Tanzania hususani kwa wafyatuaji ambao hutegemea saruji 
inayoimarika haraka katika kazi yao. “Mbali na uimara, faida nyingine ya
 Supaset ni kuweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa na maana kwamba majengo 
yatakayojengwa kwa saruji hiyo yatadumu zaidi”
Alisema
 neno Supaset linamaanisha uimara kutokana na kukauka mapema na kukaa 
muda mrefu zaidi katika uimara na saruji hiyo ni sehemu ya saruji za 
chapa ya Tembo.





Post a Comment