Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya kupitia CCM Sambwee Shitambala akizungumza mara baada yaa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi jimbo la Mbeya mjini uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura Oktoba 25 katika moja ya vituo vya kupigia kura jijini Mbeya |
Mmoja wa wapiga kura aliyejitokeza asubuhi katika moja ya kituo cha kupigia kura Oktoba 25 jijini Mbeya |
Kwanza
napenda kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia sote kumaliza kampeni
na uchaguzi kwa usalama na amani bila kuibuka kwa vurugu za aina yoyote. Na
hiii ilikuwa kauli mbiu yangu amani na usalama ndo msingi wa maendeleo ya nchi
na jimbo letu.
Pili natoa
shukurani kwa chama cha MapinduzI kwa kuniteua kupeperusha bendera ya chama
changu katika uchaguzi mkuu kugombea ubunge jimbo la Mbeya mjini ambao
ulihitimishwa Oktoba 25.
Pia
nawashukuru wanahabari kwa msaada wao katika kuujuza umma wa Mbeya mambo
yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni zetu tulizokuwa tukizifanya kwenye kata zote
36, nilifanikiwa kufanya jumla ya mikutano 56 na zaidi ndani na nje na niliweza
kukutana na wananchi wengi maeneo mbalimbali niliyofanya kampeni na kusikiliza
kero zao.
Nachukua
fursa hii pia kuwashukuru wagombea wenzangu wote wa ndani ya chama wapatao 15
kwa kushirikiana nami katika Kampeni hizo. Shukrani za pekee zimwendee Charles
Mwakipesile aliyekuwa Meneja wangu.
Pamoja na
mimi kuteuliwa na chama bado wagombea wenzangu katika chama walijitahidi
kuniunga mkono na kunisapoti kwa hali na mali wapo walioacha shughuli zao na
kuzunguka nami kwenye kampeni zote jitihada zao zimeonekana, nawashukuru sana.
Navishukuru
kipekee vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa, ngumu na nzuri
waliyoifanya na kulifanya jiji letu la Mbeya kuwa salama hadi leo. Nawashukuru
sana.
Nilijitahidi
kufanya kampeni za kistaarabu, kwa kutumia uwezo wangu wote pamoja na matukio
mbalimbali ya kejeli yaliyokuwa yakitolewa na wapinzani wetu, nilichukulia kama
ndio siasa kwani kila mmoja alikuwa anatafuta kiti cha Ubunge wa Jiji la Mbeya
kwa namna yake lengo letu lilikuwa moja kusukuma maendeleo ya Jiji letu.
Mwenzangu wa
chadema ameibuka na kura nyingi zaidi ya wengine tuliogombea naye na kutangazwa
kuwa mbunge mteule wa jiji la Mbeya. Haya ni maamuzi ya wana Mbeya wengi zaidi
ya wale waliotaka niwe mbunge wao. Nampongeza Sugu kwa ushindi huo na pia
ninamtakia kila laheri katika muda wake wa uongozI. Pamoja na dosari zilizojitokeza
kwenye uchaguzi huu lakini nimekubaliana na matokeo, tuweke mambo ya itikadi
pembeni tusimame pamoja tuijenge Mbeya yetu.
Kwa bahati
mbaya sana nimeshindwa katika uchaguzi huu nikiwa nimekusanya takribani kura
50,000 inawezekana wakati bado haujafika
wa mimi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya, nimefarijika kwa wale walionipa kura na
hata wale ambao hawakunichagua,
Nawashukuru wananchi wote.
Najua
walionichagua walinielewa, walinikubali,walihitaji niwawakilishe. Nasema
nitawawakilisha na sitowatupa. Yale niliyoyasema yatatimia juu yao kwa namna
moja ama nyingine kadri Mungu atakavyojalia. Sitawaacha wala kuwaangusha.
Nawaomba wasijione wameshindwa na wasikate tamaa. Nipo nao pamoja. Ahadi
nilizotoa wakati wa kampeni nitazitekeleza kwa kadri ambavyo Mungu atanijaalia.
Nipo na
wanajamii hapa hapa Mbeya, shughuli zangu na biashara zangu zipo hapa Mbeya
nitaendelea kuwa na wana Mbeya kwa hali na mali tukiendelea kulijenga Jiji letu
la Mbeya.
Naahidi
nitaendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo la Mbeya kwa hali na mali
nikifuatilia na kutekeleza ahadi zilizoahidiwa na Rais mteule Dkt.John Pombe
Magufuli, pamoja na kwamba sikuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Mbeya.Kwa
niaba ya walionipigia kura nitafanya kazi.
Ndugu
wanahabari nilijiwekea vipaumbele wakati wa kampeni zangu pamoja na ahadi kwa
wananchi wa jimbo la Mbeya katika baadhi ya maeneo niliahidi mambo mbalimbali
kama vile ujenzi wa zahanati kata ya Iyunga, Igawilo, Ilemi na Nsoho. Shule
kata ya Iziwa, na zinginezo, usafiri wa daladala pembezoni, maji na umeme. Pia
kutafuta waalimu wazuri kwa ajili ya shule zetu. Bila kusahau pembejeo kwa
wakati. Nitashirikiana na wananchi katika kutekeleza ahadi zangu.
Pia zipo
ahadi nilizoahidiwa na Rais wangu mteule ambaye ni muadilifu na mchapakazi
nitamkumbusha ikiwemo km 10 za barabara Jiji la Mbeya na mengineyo ambayo
nimeahidi kuyatekeleza mwenyewe kwa wapiga kura wakati wa kampeni.
Ndugu zangu
wanahabari, naamini mlikuwa mkitafakari kukaa kwangu kimya baada ya kumalizika
kwa uchaguzi huu wengi walitegemea ningeweza kupinga matokeo, kufanya hivyo
kungesababisha kuchelewesha mahitaji ya wakazi wa jiji la Mbeya ambao
wanahitaji huduma yangu na ahadi nilizotoa kwa wengi waliojitokeza kuniunga
mkono, nawaahidi sitawaangusha.
Mwisho
lakini si kwa umuhimu napenda kuwasisitiza wakazi wa Jiji la Mbeya kuendelea
kushikamana kwa ajili ya kuliendeleza jiji letu, tuepuke vishawishi na
kujiingiza katika mambo ya uvunjifu wa amani na utulivu.
Amani ya
Mbeya ikitoweka hakuna biashara inayoweza kufanywa wala hakuna shughuli zozote
za maendeleo ambazo zinaweza kufanywa,vijana wajikite kwenye ujasiriamali
watafute riziki yao halali kwa kuwa Mbeya yenye amani na salama kwa Maendeleo
yetu linawezekana.
Ahsanteni
Capt.
Sambwee Shitambala (MNEC-CCM, Mbeya)
MWISHO
Post a Comment
Post a Comment