Shilingi milioni 250 zilizopaswa kutumika kwa ajili ya
chakula kati ya Rais Dkt.Magufuli na wabunge zimeelezwa kutumika kwa ajili ya
kununulia vitanda 500 vya Hospitali ya TAIFA Muhimbili.
Kwa nia
njema kabisa rais ameamua kufanya maamuzi hayo akiamini kuwa anachokifanya
kitaisaidia jamii ya wengi wanaotaabika hospitalini kwa kulala chini na baadhi
yao kukosa dawa, Big Up Mr President!!!!.
Rais
Magufuli alihutubia bunge siku ya Ijumaa Novemba 20 ambapo baada ya kumalizika
kwa hotuba ya Spika wa Bunge Job Ndugai alisikika akiwatangazia wabunge
kuhudhuria chakula pamoja na rais hiyo ni baada ya kupata picha ya pamoja.
Imeelezwa kuwa
rais aliamua gharama za chakula hicho zilizofikia shilingi milioni 250 zielekezwe
kwenye huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya dawa na vitanda,
Shout Up Mr President kwa huruma zako kwa watanzania wenye matatizo.
Siku ya pili
baada ya kutolewa taarifa hiyo wagonjwa katika hospitali ya muhimbili walishuhudia
vitanda 500 vikiletwa hospitalini hapo.
Swali
linakuja ,Jee!! ni utaratibu upi
umetumika kwa ajili ya kupatikana kwa vitanda hivyo?sheria za manunuzi kwa
ajili ya mali za serikali zimefuatwa?
Vitanda hivyo
vimetolewa wapi kwa haraka namna hiyo na wazabuni wangapi walishindanishwa kwa ajili ya kazi hiyo ya usambazaji wa
vitanda hospitalini hapo na hatimaye mmoja akapatikana kama ambavyo taratibu za zabuni za serikali
zinavyotakiwa?
Post a Comment
Post a Comment