Diwani wa kata ya Songwe Ayasi Njalambaha akimkabidhi cheti mmoja wa maskauti waliohitimu mafunzo ya miaka miwili kambo ya Songwe Magereza |
Diwani wa kata ya Songwe Ayasi Njalambaha akitoa nasaha baada ya kukabidhi vyeti vya mafunzo kwa wahitimu wa Skauti Songwe |
Baadhi ya Skauti waliohitimu mafunzo ya skauti jana |
Kaimu Mkuu wa magereza wa Songwe Saleh Hassan akitoa nasaaha wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti maskauti waliohitimu mafunzo ya miaka miwili jana |
Mkufunzi wa mafunzo ya Skauti Deogratius Mazengo akimkaribisha mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Songwe Ayasi Njalambaha kwa ajili ya kitendo cha kuapisha wahitumu wa mafunzo ya Skauti. |
WAHITIMU wa
mafunzo ya miaka miwili ya Skauti wilayani Mbeya wametakiwa kutumia mafunzo ya
miaka miwili waliyopata kwa kulinda amani na utulivu wa nchi yetu ikiwa ni
pamoja na kutojiingiza katika vikundi vya uhalifu.
‘’Mafunzo
yenu yalenge kuisadia jamii na kutumia mbinu mlizopata kwa ajili ya kujiletea
maendeleo yenu wenyewe’’alisema Diwani wa Kata ya Songwe Ayasi Njalambaha.
Njalambaha
pia aliwataka wahitimu hao kumtanguliza Mungu katika utendaji wao katika jamii
ili kujijengea imani ya Mwenyezi Mungu na kuwa daima kila mwenye imani hutenda
haki.
‘’Mtangulizeni
Mungu kwenye kazi zenu huko mbele ya jamii, ukimtanguliza Mungu utakuwa na
imani, ukiwa na imani utatenda haki, tunaporudi katika maeneo yetu tusaidie
kudumisha amani na utulivu,’’alisema Njalambaha.
Aidha
Njalambaha aliwaasa wahitimu hao kutojihusisha na ubaguzi unaohusisha makundi ya itikadi za kisiasa ama ya kidini na
kwamba wanatakiwa kutanguliza uzalendo na kusaidia maendeleo ya nchi yetu bila
ubaguzi.
Kwa upande
wake Kaimu Mkuu wa Magereza wa Gereza la Songwe Salehe Hassan Saleh aliwataka
wazazi kutoa ushirikiano kwa vijana wanaojiunga kwenye mafunzo ya Skauti kwa
kuwa mafunzo hayo mbali na kuwajengea uwezo na uelewa huwapa ujasiri na
ukakamavu.
Naye
Mkufunzi wa mafunzo hayo Deodatus Mazengo alisema kuwa mafunzo hayo
yaliwahusisha skauti 47 waliopata mafunzo ya miaka miwili ambao wametokea katika vijiji vilivyopo kata ya
songwe wilaya ya Mbeya.
Post a Comment
Post a Comment