NI tukio la kutisha katika historia ya medani ya soka duniani nchini Argentina baada ya mchezaji mmoja kumuua uwanjani kwa kumfyatulia risasi tatu refarii Cesar Flores na hatimaye kukimbia.
Imeripotiwa kuwa tukio hilo limetokea wilayani Cordoba baada ya mwanasoka huyo kuoneshwa kadi nyekundu na Flores kutokana na kumpiga mchezaji wa timu pinzanidakika za mwanzo za mchezo.
Polisi nchini Argentina imethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mchezaji huyo baada ya kumpiga risasi Flores kichwani, shingoni na kifuani alimlenga mchezaji mwingine Walter Zarate ambaye alijeruhiwa na hali yake inaelezwa kuwa sio mbaya.
Taarifa inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati wa mechi na kuwa haijulikani ni nini zaidi kilitokea kati ya mchezaji huyo na mwamuzi bali mchezaji alikasirika na kwenda kuchukua bunduki yake ndani ya mkoba wake na kumuua mwamuzi.
‘’ “Yote hayo yametokea wakati wa mechi,” alisema msemaji wa polisi. “Hatujui nini kilitokea kati yake na refarii, lakini mchezaji alikasirika na kwenda kuchukua bunduki yake na kumuua.” Mwanasoka huyo ambaye alikuwa na silaha hiyo ndani ya mkoba wake, anatafutwa na polisi baada ya kukimbia.
Post a Comment
Post a Comment