Ads (728x90)

Washitakiwa wa kesi ya kuchoma Kor an tukufu wakiingia katika mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya kosa linalowakabili
Mshitakiwa nambari moja wa kosa la kuchoma Kor an akiwa sakafuni baada ya kuangula kizimbani kabla ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo

Baadhi ya akina mama waumini wa dini ya Kiislamu wakiingia mahakamani kusikiliza kesi ya uchomaji Kor ani
Washitakiwa wa kesi ya uchomaji Kor an kabla ya kupanda kizimbani mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Namtumbo kusikiliza kesi inayowakabili
Mshtakiwa wa kesi ya uchomaji Kor an Rashid Ausi akisaidiwa kupelekwa Hospitali baada ya kuanguka kizimbani kabla ya kusomewa mashtaka yanayowaka
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye kikao cha dharura kwenye ofisi ya BAKWATA iliyopo msikiti mkuu wa wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uchomaji wa Kor ani
Baadhi ya waumini wa Kiislamu akina mama wakishiriki kikao cha dharura mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uchomaji Kor ani kwenye mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo
Washitakiwa wa kosa la kuchoma Kor ani wakiwa kizimbani ndani ya Mahakama ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
Baadhi ya waumini wa Kiislamu wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uchomaji wa Kor an
 
Taharuki imeibuka katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Namtumbo baada ya mshitakiwa namba moja kati ya washitakiwa sita wa kesi ya jinai namba 48 ya mwaka 2016 kuanguka kizimbani  na hivyo kulazimika Hakimu wa Mahakama hiyo Majinge Kusaga kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21.

Hali iliyoibua taharuki mahakamani hapo imetokana na  mshitakiwa huyo Rashid Ausi(75) ambaye ndiye mshitakiwa nambari moja mara baada ya kupandishwa kizimbani alionesha dalili za kuishiwa nguvu na kunyong’onyea huku akijitahidi kunyoosha mkono wake ili aruhusiwe kuzungumza chochote.

Mara baada ya Hakimu kumruhusu kusema akazungumza kwa taabu maneno mawili ‘NATAKA KULALA’  kama vile hakusikia vyema alichosema mshitakiwa huyo alimtaka mshitakiwa kurudia tena kueleza tatizo lake mara ya pili, kabla hajajibu kwa ufasaha alichohitaji  mshitakiwa huyo alianguka chini na kulala kizimbani na baadaye kubebwa na kulazwa pembeni kabla ya kusindikizwa Hospitali ya wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Maneno yake yaliyosikika kwa uchache kutoka kinywani mwake yalikuwa ni kwamba anajisikia tumbo linamuuma na hata walipotakiwa baadhi ya jamaa walioambatana naye wamsindikize chooni, mshitakiwa huyo alilala pembeni ya benchi lililopo mahakamani humo ambapo wakati huo huo Hakimu aliomba kuahirisha kesi hiyo kwa dakika 10 ambapo aliwataka jamaa wa mshitakiwa kumpeleka hospitali mshitakiwa huyo. 

Wakati mshtakiwa huyo akipelekwa hospitalini Hakimu Kusaga alitamka kuiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21 ambapo upande wa Mashtaka utawaleta mashahidi wa kosa hilo linalowahusu washitakiwa 6 ambao wanadaiwa kuteketeza kwa moto vitabu vya dini ya Kiislamu (Koran) kutokana na  shinikizo la imani za ushirikina.

Awali washitakiwa 6 wamefikishwa mahakamani hapo wakituhumiwa kwa kosa la kuchoma Kor ani Tukufu,Kitabu kinachotumiwa na waumini wa dini ya Kiislamu wakishtakiwa kwa kosa la kuharibu mali na kumuita mtu mchawi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea katika kijiji cha Ngwinde Kata ya Litola wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo washitakiwa hao Rashid Ausi(75)Shazir Rashid(31)Rashid Nchimbi(35)Abdalla Nchimbi(56)Kanuti Nchimbi(53) NA Juma Ndembo(36) wanakabiliwa na mashtaka hayo.

Eneo la Mahakama ya wilaya ya Namtumbo lilihudhuriwa na umati wa waumini wa dini ya kiislamu hali ambayo haijawahi kutokea katika wakati mwingine na hivyo kuibua zaidi taharuki miongoni mwa watu waliokusanyika mahakamani hapo kusikiliza kesi zingine.

Post a Comment

Post a Comment