Ads (728x90)

Binadamu na mtu yote ni majina ambayo amepewa kiumbe aliyeumbwa na na Mola na kupewa utashi wa kujua zuri na baya na kumaizi yanayojiri kwa matlaba ya kuishi vyema na vimbe wa aina yake na wale wanaoshabihiana naye katika dunia.

Ni jambo la aibu kuona binadamu anauvua utu wake na kudiriki kujamiina na binadamu mwenzie kinyume na maumbile ambapo si hivyo tu bali binadamu hao wamevuka hali ya ubinadamu na kujivika unyama na kwa kujamiina na wanyama seuze watoto wadogo vichanga...inatia aibu.

Huwa nakaa na kutafakari hatima ya sisi tunaojiita binadamu wenye utu kwa vitendo hivi vinavyozidi unyama,haya mambo asili yake ni wapi na ni kwa nini uwepo unyama wa aina hii.

Limekuwa ni jambo la kawaida kila uchao kusikia mara ooh! babu fulani kambaka binti mdogo mwenye umri wa miaka miwili au minne tena pia si ajabu kusikia kwamba kuna mtu kabambwa akimpanda kuku au ng'ombe,hata kule Mbozi mkoani Mbeya ilipata kutokea jamaa akatengeneza jiwe lililoshabihiana na maumbile ya sehemu za siri za mwanamke na kutumia fursa hiyo kuliingilia jiwe hilo na hatimaye kupata madhara katika sehemu zake za siri.

Jamaa huyo ilidaiwa alifanya hivyo kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa wa UKIMWI lakini je ni kweli inakuja akilini kwamba aliyefanya kitendo kile ana akili timamu?tunaweza kumsifu jamaa huyo lakini hebu na tujiulize hii amri ya watawa kutoolewa na kutooa ina madhara gani kwa jamii?

Naamini maumbile ya binadamu huenda kulingana na jinsi Mwenyezi Mungu alivyotaka yawe sasa iwapo kuna baadhi ya madhehebu yanashiniza watu wasioe au kuolewa nini mantiki yake hapa, inawezekana hili jambo ndilo linaloshawishi vitendo vya kinyama vikashamiri

Wakatabahu kazi kwenu wachangiaji

Post a Comment

  1. Suala la kuwa tumezaliwa tukiwa na uwezo wa kujua mema na mabaya nimekuwa nalifikiria sana siku za karibuni. Hivi ni kweli tunazaliwa na uwezo huu au mazingira na utamaduni ndio vinatufunza lipi jema na lipi baya?

    ReplyDelete