Maisha ya binadamu hutegemeana kihali, kulingana na tofauti ya maisha kati ya mtu na mtu,uwiano wa kipato baina ya watu aina mbalimbali ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu,hivyo kipato cha mmoja si sababu ya wengine kujiona kwamba wamemkosea Mwenyezi Mungu bali huo ni mpangilio maalum wa maisha ili dunia iweze kwenda.
Ama kwa wale ambao wamekosa kipato au hali zao ni za kijungu jiko ambao hutegemea kupata riziki ya siku moja ilhali ya siku inayofuata ni majaliwa hawana budi kufanya bidii katika kujishughulisha na maisha bila kukata tamaa kwani mtoaji wa riziki ni mmoja tu, hakuna yoyote anayeweza kutamba kuwa ana uwezo wa kugawa ama kuzuia riziki ya mtu zaidi ya Mwenyezi Mungu ambaye kila mwanadamu amempangia riziki yake kwa wakati wake maaluma tangu alipozaliwa hadi siku ambayo ataiaga dunia.
Ni jukumu la kila mwanadamu kujifahamu na kujitambua umuhimu wake wa kuwepo katika dunia ambapo matumaini ya maisha yake huenda mnasaba na matendo yake ya maisha ya kila siku.
Wakatabahu.
hii ni kazi makini,
ReplyDeletetumuombe maanani,
atupe nguvu zaidi,
ili kitoke utumwani.
Nashukuru kwa ujumbe wako ni matarajio, sote tuishio chini ya anga hili la wadudi, tunawiana kimawazo isipokuwa tunahitilafiana kimatendo kulingana na upeo wa fikra zetu na mtazamo wa kila mmoja kulingana na wakati au mahali anapoishi.
ReplyDeleteWakatabahu.
Hatua za maisha ya mwanadamu ni majaliwa ya mwenyezi mungu tangu kuzaliwa, kukua na kufa.
ReplyDeleteTabia za vitendo vya binadamu vimekithiri uovu kiasi cha kujisahau kwamba tumeumbwa na iko siku tutakufa.
Vitendo vya binadamu kumuasi Mola ilhali tunakula na kunywa kutokana na rizki iliyotokana na Mwenyezi Mungu ni Ibra ambayo inatakiwa kila mwanadamu ajifunze kwayo.
Kwani iwapo sisi wanadamu tunatakabari juu ya mgongo huu wa ardhi ilhali siku moja tutakuwa ndani ya shimo tukiliwa na wadudu, kwanini basi tusijiongezee umri wa kuishi wakati tunakaribia kuiaga dunia?
Hiki chote ni kiburi ambacho hakina maana yoyote, kwani chakula tulacho, hewa tuvutayo na mengine mengi ni kudra za mola zisizohesabika, hivyo basi ni wajibu wa mwanadamu kufikiria atokako na kule aendako na kutafakari mustakabali wake baada ya kuiaga dunia.
Wakatabahu
Mtu mwema hudhihirika kwa vitendo vyake kadhalika kwa mui vivyo hivyo, bali kwa mtu mwema vitendo vyake hupaliliwa na kumea katika ardhi njema iliyotiwa mbolea ya maneno yaliyojaa busara na utukufu wa matumaini mema ya maisha katika dunia.
ReplyDeleteWatendao wema daima haweshi dawamu, bali mola huwachukua mapema ili wasikhasiriwe na maovu yaliyokithiri chini ya anga hili lenye misuto, kebehi na bezo lukuki za wanadamu waovu.
Ama watendao maovu Mola huwaacha wapate fursa ya kutubia kwa kila baya walitendalo asaa wanaweza kujirekebisha kutokana na maovu yaliyokithiri katika darmadar ya maisha yao ya kila siku.
Ni matarajio ya sisi viumbwa kuwa wanyenyekevu na wasikivu juu ya utashi wa kile ambacho Mungu ameamrisha kwa wanadamu kukifanya kila siku ikiwa ni pamoja na kuepuka maovu na kutenda yaliyo mema.
Wakatabahu